Aliyekuwa Kocha wa viungo na Saikolojia wa Timu ya Simba, Syllersaid Mziray 'Mwanangu' amefariki dunia usiku wa kuamkia leo imefahamika.Hadi mauti yanamfika hali yake ilikuwa mbaya huku akiwa amelazwa katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) katika Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam sambamba na kuwekewa mipira maalum kwa ajili ya kumsaidia kupumua.Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Kaburu Nyange amesema kwa niaba ya uongozi wa Klabu yake wamepokea msimba wa aliyekuwa Kocha wa viongo na Saikoljia wa timu ya Simba Super Coach SyllerSaid Mziray aliyefariki dunia jana alfajiri.
Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam Nyange amesema kwamba mwili wa marehemu Mziray utapumzishwa katika nyumba yake ya milele Jumatatu huku msiba ukiwa nyumbani kwake Tabata Magengeni Jijini Dar es Salaam.
Aidha Nyange aliongeza kwa kusema kuwa wao kama viongozi wa Simba walijitahidi katika kumhudumia marehemu Mziray wakati alipokuwa mgionjwa lakini yote yaliyotokea ni mapenzi ya mungu hivyo aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi.
Mziray alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu Huria atakumbukwa kwa umahiri wake katika ufundishaji wa soka katika vilabu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuleta ushindi kupittia timu ya taifa iliyoshinda ubingwa wan chi za Afrika Mashariki. Timu alizofundisha enzi za uhai wake ni Pilsner, Simba Yanga Pam African. Ameacha mke na watoto Mungu aipumzishe roho yake kwa amani. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimdiwe AMEN.
Biashara : NMB Yaleta Nondo za Pesa kwa Watanzania
-
KATIKA kuongeza uelewa wa masuala ya fedha kwa maendeleo na ukuaji kiuchumi
kwa Mtanzania mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla, Benki ya NMB imezindua
Progra...
Cara Terbaik Untuk Menang Judi Sicbo Online
-
Bergabung dalam permainan judi sicbo online yang dapat dimainkan melalui
smartphone, maka tentu saja para pemain bisa melakukan sejumlah taruhan
dengan nya...
Waziri Ndalichako azindua chuo kipya cha VETA Kagera
-
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amezindua
chuo kipya cha VETA Ndolage kilichopo Kamachumu Wilaya ya Muleba mkoani
Kagera k...
0 Comments