Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel Mpangala pichani juu baadaye leo atapanda jukwaani kuwakilisha nchi katika shindano la kumsaka mrembo wa dunia Miss World 2010, katika shindano lililopangwa kufanyika katika kisiwa cha Hinan Sanya China.
Mpaka sasa mrembo huyo ameshindwa kuingia katika 22 bora za shindano hilo na kukosa mataji mengine madogo yanayoshindaniwa.Genevive atashangiliwa na msafara wa watu 5 ukiongozwa na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga waliondoka nchini Oktoba 25-2010 kwenda Sanya China katika kuhudhuria mashindano hayo.
Pia katika ujumbe huo yumo Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania Bosco Majaliwa, Mshindi wa 2 wa Mis Tanzania Glory Mwanga na Miss Temeke namba 2 Anna Daudi ambaye pia alifanikiwa kuingia katika 10 bora ya Fainali za Miss Tanzania 2010.
Aidha Mama Mzazi wa Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel, Mrs. Mary Mpangala leo atamshuhudia binti yake akipanda katika jukwaa la kimataifa.Wote wanaatarajiwa kurudi nchini Novemba 3 2010.
RC SIMIYU AANZA ZIARA YA SIKU 30 KWA KISHINDO KIJIJI KWA KIJIJI
-
Na Mwandishi Wetu,Simiyu
MKUU wa Mkoa wa Simiyu Mkuu Kenani Kihongosi amesema Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amewaagiza vi...
1 hour ago
0 Comments