UJUMBE WA WATOTO WATEMBELEA FAMILIA ZILIZOPATA MSIBA WA WATOTO TEMEKE

Na Andrew Chale

Ujumbe maalum wa watoto nchini umetembelea ndugu na jamaa waliopatwa na msiba kufuatia hitilafu ya umeme kwenye ukumbi wa Luxury Pub Temeke na kusababisha vifo vya watoto watatu.Ujumbe huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea haki za watoto nchini, Nimka Lameck (11), Salome Filbert (7), Monica Ntevi. Joseph Nzozi na Maleo Lameck.Walitembelea familia ya Mtoto Fatuma Ramadhani (7) ambaye alifariki dunia papo hapo ukumbini humo ambapo mama yake Zaituni Chenja ambapo alionekana na huzuni huku akisema anamwachia Mungu.Pia walitembelea familia mbili na kutoa rambirambi kwa wafiwa pamoja na kutoa ujumbe wa kuwafariji wafiwa hao kwani yaliyotokea ni mapenzi ya Mungu.“Sisi watoto pamoja na wenzetu tumewakilisha tunatoa pole sana kwani tumeguswa na tatizo hili kwa ujumla tunaomba sheria kali zichukuliwe dhidi ya wahusika” walisema watoto hao.Aidha, ujumbe huo pia ulitoa rambirambi zao kwa familia ya Lilian Rajabu (9) ambaye naye alizikwa juzi na walitoa pole kwa ndugu na jamaa sambamba na kutoa ubani wao.Hata hivyo ujumbe huo ulitembelea ukumbi wa Luxury Pub na kujionea jinsi palivyo, ambapo walitoa sala zao na kukemea vikali kwa tukio hilo. Baadhi ya watoto ambao walishuhudia tukio hilo.Walitoa maoni yao na kuomba Serikali kuimarisha ulinzi katika siku za sikukuu kwenye baa na kumbi za starehe ili kupunguza matatizo kama haya yanayotokea kwa watoto.“Tunakumbuka mwaka 2008, tukio kama hili lilitokea na kusababisha vifo kwa watoto 19, katika ukumbi wa Bubbles Mkoani Tabora, hivyo hatutaki tena kushuhudi vifo vya watoto wenzetu vikiendelea kwani hawana hatia” walisema baadhi ya watoto waliokuwa na umri kati ya miaka 15 -17 ambao ni wanafunzi wa kidato cha pili na tatu na wakazi wa Temeke.Mmiliki wa Luxury Pub anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi.
Ukumbi wa Luxury Pub ambako maafa yalitokea katika sikukuu ya Eid El Fitr.
Nimka na msafara wake wakiwasili Luxury Pub.
Mwandishi na Mwanaharakati wa masuala ya watoto kwa ujumla Andrew Chale naye alikuwepo katika ziara hiyo jana.




Nimka akiwafiriji wazazi.

Post a Comment

0 Comments