TAMASHA la 29 la Sanaa linaloandaliwa chini ya Mwamvuli wa Taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TASUBA) iliyo chini ya Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo ni mojawapo ya matamasha nguli hapa nchini yenye mrengo wa kufanikisha safari ya tasnia hiyo hapa nchini.Tamasha la mwaka huu lenye kauli mbiu ‘Sanaa na Utamaduni katika kuimarisha Demokrasia’ ikiwa na lengo la kuhamasisha uchaguzi Mkuu wa mwaka huu linatarajia kuanza Septemba 27-Oktoba 2, ambapo litafanyika chuoni hapo.Vikundi vitakavyoshiriki tamasha hilo ni Wanguu, Uhuru Youth Centre, Shada Jah Man cha Bagamoyo, Man Kifimbo cha Kimanzichana, Town Shakers, Totoo Niwenhuiti cha Rwanda, Splendid Dar es Salaam, Chibita cha Bagamoyo, River Nile cha Zanzibarr, Dira, Chief Cultural Group, Youth Movement For Change cha Singida. Vingine ni Dogodogo Centre cha Kigogo, Mwenge Sanaa cha Tabora, River Nile cha Dar es Salaam, Dira cha Mwanza, Inshoza cha Rwanda, Tongwa Ensamble cha Norway, Imara Boma Dar es Salaam, Chibite Group cha Bagamoyo, Cocodo Traditional cha Dar es Salaam, Nyuki cha Songea na Kilimanjaro Wizards cha Moshi.Msambo Art Goup cha Morogoro, Kituo cha Utetezi wa maendeleo ya walemavu Dar es Salaam, Nyota Kali cha Dar es Salaam, Buyegu cha Mwanza, , Maembe, Jua Children vyote vya Bagamoyo, Mbudye Balondo cha Congo DRC, Kizingo Arts cha Kenya na vinginevyo.Bafadhili anasema ushiriki wa tamasha la sanaa Bagamoyo hakuna masharti ambako alitoa wito kwa wasanii wa nyanja zote kujitokeza kushiriki klwa matamasha yanayokuja kwa sababu tamasha hilo ni la kwao anatoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kudhamini tamasha hilo ambalo ni mojawapo ya matamasha makubwa hapa nchini.

Post a Comment

0 Comments