SERIKALI kwa kupitia Wizara ya Habari Michezo na utamaduni wametoa cgangamoto kwa warembo wanaoshiriki kinyang’anyiro cha kumtafuta Vodacom Miss Tanzania 2010 kutumia lugha adhimu ya Kiswahili popote pale watakapokwenda.Rai hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari Michezo na Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko wakati alipokwenda kuwatembelea warembo hao ambao wako kambini katika hoteli ya Giraffe View Jijini Dar es Salaam. “Tumiemini lugha ya Kiswahili kwa sababu ina hadhi na kutambulika kote ulimwenguni , tumieni lugha hii na mjisikie huru popote pale mtakapokwenda kwani hata Shirika la Elimu na Utamaduni Duniani UNESCO wmetoa takwimu kwamba lugha ya Kiswahili inatumiwa na watu zaidi ya milioni 180” alisema Mwansoko.Aliongeza kwa kusema kuwa “Jivunieni Kiswahili huu ndiyo utambulisho wetu wa msishikwe na vigugumizi pia katika ubinifu wenu tumieni chombezeni Utanzabnia ndani yakeili tujitangaze vyema” alisema.Aidha Mwansoko aliwapongeza waandaaji kwa kuwa na washiriki bomba, huku akiwapongeza warembo wenyewe na kuwaambia kwa kuwa wote wako kambini kwa ajili ya shindano hilo la Taifa hivyo wote ni washindi.Mwansoko aliongeza kwa kusema kuwa urembo ni sanaa kamili ambayo Mtanzania yeyote anapaswa kujivunia.Wakati huohuo naye Chiku Shomari ambaye alikuwemo katika msfara huo aliwaasa warembo hao wametakiwa kufuata maadili mema, kujitambua, kujithamini na kujipenda kwani huo ndiyo msingi wa kupata maendeleo kwa mtoto wa kike popote atakapokuwa.Shindano la Vodacom Miss Tanzania limepangwa kufanyika Septemba 11 mwaka huu.
Rais Samia ahutubia Mabalozi ,Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika
Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu Jijini
Dar
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa
kwenye Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu...
10 hours ago
0 Comments