RASCOM kukutana leo

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Satelite Afrika (RASCOM) Bw. Jones Killimbe (pichani) akizungumza jana waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu mkutano wa bodi wa RASCOM utakaofanyika leo.
Ambapo nchi za Afrika zimetakiwa kuboresha mawasiliano kwa njia ya satelite ili kukuza mawasiliano ya uchumi, hayo yalisemwa na Killimbe kuwa mawasiliano hayo yamesaidia kuboresha huduma za jamii.Katika Mkutano wa leo bodi ya RASCOM itazungumzia mafanikio toka walipoanza kutoa huduma za Satelite . Na kuoongeza kuwa matumizi ya mawasiliano kwa njia ya satelite yatasaidia kuboresha huduma za Benki na kurushwa kwa matangazo ya Redio na Televisheni kwa urahisi zaidi .Aidha Killimbe alisema 65% ya wananchi wanaoishi vijijini nao wanahitaji huduma za mawasiliano ili kuwa na maisha bora RASCOM itasaidia kuunganisha zaidi ya shule 600,000 za Afrika ili kuongeza ufanisi kwa wanafunzi.

Post a Comment

0 Comments