
Queen Suzy ambaye ni mnenguaji bab'kubwa Bongo akiwa sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka wengine ni Aisha Madinda na Mandela wote ni wanenguaji wa bendi hiyo wakifurahi pamoja baada ya onyesho la bonanza linalofanyika Leaders Club Kinondoni Dar es Salaam.

Mimi nikiwa na mtani wangu Amos Msanjia ambaye ni Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza hivi sasa amekuja nchini kwa mapumziko mafupi na anaye fuata Mkurugezi mdogo wa bendi ya The African Stars Twanga Pepet Aziza Baraka 'Aunt Aziza'.

Stori zilikuwa kibaooo.

Macho mbele kwenye jukwaa tukiangalia wanamuziki wa bendi ya Twanga wakikamua.

Ni wakati wa mishkaki sasa.
0 Comments