BASATA yataja Majina ya Majaji 9 Miss Tanzania .

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA),jana limeteua majina tisa ya majaji watakao husika katika kumchagua mshindi wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010. Majaji waliochaguliwa ni jina na kazi yake kwenye mabano Richard Magongo (Group InternalAudit Manager Tanzania Breweries),Bernad Mrunya (Chief Conservarto Ngorongor Crater Authority),Devota Mdachi (Mkuu wa Kitengo Cha Habari za Utalii-TTB),Ayubu Rioba (Mwenyekiti MISA),Michale Shilla(Director Corporate &Consummers Affair Competition Commission), Basila Mwanukuzi (Alikuwa Miss Tanzania 1998), John Njoroge raia wa Kenya (General Manager Corridor Spring Hotel –Arusha),Stella Kiwango (Mkurugenzi Uajiri Vodacom) na Prashant Patel (Mwenyekiti Kamati ya Miss Tanzania). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kampuni ya Lino International Agency ambao ndiyo waratibu wa shindano hilo ilisema kanuni , sheria na taratibu za mashindano ya urembo ya Miss Tanzania Kamati ya MissTanzania hupendekeza majina 15 ya wadau wa sanaa ya urembo wakiwemo wadhamini pamoja na wadau wengine ambapo BASATA huteua majina tisa. Baada ya uteuzi huo majaji hupewa semina na utaratibu wa mashindano haya na baadaye kushiriki katika shughuli ya kumchagua mrembo wa Taifa atakaye wakilisha nchi katika mashindano ya dunia.Wakati huohuo wasanii Wahuu, bendi ya Tanzanite, Ambwene Yessaiyah watatumbuiza katika shindano hilo lililopangwa kufanyika Mlimani City Septemba 11.

Post a Comment

0 Comments