MUIMBAJI mwenye sauti ya aina yake Salehe Kupaza , amesimamishwa kazi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The African Stars (ASET) Asha Baraka ,inayomiliki bendi kongwe ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta International.
Kusimamishwa kazi kwa muimbaji huyo kunatokana na kosa la utovu wa nidhamu aliouonesha mbele ya Mkurugenzi wake.
Akizungumza na Bongoweekend Asha alisema kwamba ametoa amri asimamishe ili kujifunza adabu mpakaatakavyoambiwa vinginevyo.
Äliongeza kwa kusema kwamba kumsimamisha kazi Kupaza ni njia mojawapo katika kumwonesha kwamba anawajibu wa kumuheshimu yeye kama Mkurugenzi wake.Kupaza amekumbana na kibano hicho baada ya kumtusi bosi wake ikiwa ni bada ya kuhojiwa juu ya uchelewaji kazini kutoroka mazoezini na kwenda katika mazoezi ya bendi ya Victoria na kuomba kazi .Pia aliwatukana wanamuziki wenzake .Adhabu hiyo ameanza kuitumikia kuanzia Jumatatu Septemba 23 bada ya kizaazaa kilichotokea kwenye ofisi za ASET zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam-
Maisha : Naibu Waziri Kisuo Aitaka OSHA Kutoa Elimu Endelevu kwa
Wafanyabiashara Ndogo
-
Awasisitiza Wafanyabiashara Kulinda Amani ya Tanzania
Na: OWM - KAM
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Rahma
Kisuo amei...
31 minutes ago

0 Comments