Social Icons

Tuesday, August 13, 2013

MWANAMITINDO FLAVIANA MATATA AENDELEA KUTESA KIMATAIFA

NYOTA ya mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata, imezidi kung’ara baada ya kuingia katika orodha ya wanamitindo saba bora kwa upande wa kipato.
Kwa mujibu wa gazeti la biashara la kimataifa la Forbes Africa, lililotolewa hivi karibuni, Flaviana ni mrembo pekee aliyeingia katika orodha hiyo kwa wanamitindo wa Afrika Mashariki na kuzidi kuipeperusha vema bendera ya Tanzania kimataifa.
Katika orodha hiyo, mwanamitindo Maria Borges wa Angola ndiye kinara na wengine sita pamoja na Flaviana, wakibaki kutoa ushindani mkubwa kwa mlimbwende huyo.
Mbali ya Flaviana, wanamitindo walioko katika orodha hiyo ni Candice Swaenpoel, Katryn Kruger wa Afrika Kusini, Ajak Deng, Grace Bol kutoka Sudan na Liya Kebede wa Ethiopia.
Flaviana, aliibuka katika jukwaa la kimataifa kama Miss Universe Tanzania mwaka 2007 na aliweka historia kwa kuingia 10 bora ambapo baada ya kumaliza muda wake, aliendelea na fani ya uanamitindo Afrika Kusini na baadaye alipata nafasi ya kufanya kazi Marekani na Ulaya katika kampuni kubwa ya Next Models International na sasa yuko Wilhelmina Models.
Kwa mujibu wa Flaviana ambaye hivi sasa yuko New York, amefurahia mafanikio haya na kuongeza kuwa mpango wake ni kuzidi kumweka Mungu mbele na kuhakikisha kuwa anajitahidi kadiri ya uwezo wake na kuiletea sifa familia na nchi yake.
 

No comments:

 
 
Blogger Templates