UAE YATOA MSAADA KWA WATOTO 5000 TANZANIA



 Mgeni Rasmi katika hafla  ya utoaji wa msaada , Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi (kulia) akitoa hotuba katika hafla hiyo leo jijinji Dar es salaam (kushoto) ni Sheikh  wa Mkoa wa Dar es Salaaam, Alhadi Mussa Salum. Katika hafla hiyo, UAE imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa jumla ya watoto 5000 wa nchini Tanzania.
 Baadhi ya watoto waliohudhuria katika hafla leo jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Waziri wa  Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ,Bibi Kijakazi Mtengwa akisoma risala katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akimpongeza  mtoto baada ya kumpatia msaada wa  nguo na viatu uliotolewa na  Mf uko wa kusaidia watoto  wenye mahitaji maalumu kutoka  Umoja wa nchi za Kiarabu (UAE )Charity.leo jijini Dare es salaam.(pichani kushoto) ni  Mwenyekiti wa Mamlaka ya masuala ya Kiislam na Mjumbe wa Bodi ya Red Cresent Dkt. Hamdan Al- Mazroei na (kulia)Mwakilishi wa Balozi wa UAE nchini Tanzania  Mohamed Alzaabi.
 Rais Msataafu Alhaj Hassan Mwinyi (mwenyekoti jeusi) , Mwenyekiti  wa  The General Authority for Islamic Affairs And Endowments na Mjumbe wa Bodi ya Red Crescent kutoka UAE Dkt. Hamdan Al Mazroei (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Balozi wa UAE nchini  Bw, Mohamed Alzaabi (kulia) wakiwapongeza baadhi ya watoto baada ya kuwakabidhi msaada wa nguo na viatu leo jijini . Jumla ya watoto 5000 watapata msaada huo ikiwemo mikoa ya DSm 1500.Arusha 1500, Tanga 1000 na Zanzibar 1500. 
  Baadhi ya watoto wakiingia katika jengo la Ubalozi wa UAE nchini Tanzania kuhudhuria hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa Mamlaka ya Masuala ya Kiislam na Mjumbe wa Bodi ya Red Crescent kutoka UAE akiongea leo katika hafla ya kuwakabidhi msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu nchini Tanzania, Jumla ya watoto 5000 wamebahatika kupata msaada huo wa nguo na viatu, Mfuko  wa kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu ulianzishwa  tarehe 19 mei ,2007 na Makamu wa Rais wa UAE Shaikh, Muhammed bin Rashid Al Maktoum, ukiwa na thamani ya dola za kimarekani 10 bilioni. 
Mwenyekiti wa  Mamlaka ya masuala ya Kiislam na mjumbe wa Bodi ya Red Crescent Dkt. Hamdan Al- Mazroei (kulia) akiwapa msaada wa nguo na viatu wanafunzi wa Alkhairat Islamic Center ya Mabagala jijini Dar es Salaam ,leo katika hafla hiyo ambapo mgeni Rasmi alikuwaRais Msataafu Mzee Ali Hassan Mwinyi (hayupo pichani) PICHA ZOTE NA MWANAKOMBO JUMAA-MAELEZO.

Post a Comment

0 Comments