Mkuu wa
Wilaya ya Moshi, Dr.Ibrahim Msengi(wa pili kulia) akimkabidhi Meneja wa Bar ya
East Africa,Godfrey Mawala(kulia)Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,
Oscar Shelukindo.Wapili kulia ni Mpishi Mkuu Wilfred William na Meneja Mauzo wa
Moshi, Edmundi Rutaraka
Mashabiki wa
Bar ya East Africa wakishangilia mara baada ya kutangazwa washindi wakati wa
shindano la Safari Nyama Choma lililofanyika katika Viwanja vya CCM Mkoa
Mwishoni mwa wiki.
EAST AFRICA BAR, wametwaa ubingwa wa
mashindano ya Nyama Choma Mkoa wa Moshi, baada ya kuzigaragaza baa nne
zilizotinga fainali ya mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) kupitia bia ya Safari Lager.
Kwa kutwaa ubingwa huo katika fainali
zilizofanyika juzi Jumapili kwenye Viwanja vya CCM Mkoa , baa hiyo ilizawadiwa
fedha taslim Sh milioni moja pamoja na cheti.
Waliokuwa mabingwa watetezi wa mashindano
hayo mkoani hapa, Makanyaga Bar, walishika nafasi ya pili na kuondoka na kitita
cha Sh 800,000 na cheti, wakati White Star Pub walishika nafasi ya tatu na
kupata zawadi ya Sh 600,000 na cheti.
Walioibuka na nafasi ya nne ni baa ya
Forest Bar iliyozawadiwa Sh 400,000 na cheti, wakati baa ya Lamina ilishika
nafasi ya tano na kuzawadiwa Sh 200,000 na cheti.
Akizungumza kabla ya kumtangaza mshindi,
Jaji Mkuu wa fainali hizo, Douglas Sakibu, alisema kuwa walitoa mafunzo kwa baa
zote hizo juu ya mambo wanayopaswa kuzingatia katika uchomaji nyama.
Alivitaja vigezo walivyotumia kupata
mshindi kuwa ni usafi wa mchomaji, vifaa na mazingira, maandalizi ya nyama
kuanzia uchaguzi, uhifadhi wake na wa vifaa.
Vingine ni uchomaji na upangaji nyama,
ladha na ulaini wake, mazingira ya eneo, mtiririko wa maji na uhifadhi wa taka.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, alisema kuwa ni fahari
kubwa kwa TBL na bia ya Safari Lager kwa ujumla kufanikisha shindano hilo
mkoani ambao ndio mkoa wa mwisho.
“Tulianza kwa kuwataka watu wapige kura
kupendekeza baa zinazofaa kuingia katika shindano la nyama choma kwa mkoa huu
wa Moshi tukapata baa hizi tano zilizoingia fainali ambapo leo tutampata
mshindi.
“Tunajua watu huwa wanakwenda katika baa na
kula nyama hivyo tukaona ni vema tuanzishe mashindano haya ili walaji nyama
choma wapate nyama bora,” alisema.
Alisema kuwa bia ya Safari Lager ina miaka
takriani 36 na bado imeendelea kuwapo hadi sasa ambapo ndio inayoongoza
kwa mauzo.
Kwa upande wake, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu
wa Wilaya ya Moshi, Dr.Ibrahim Msengi, aliisifu TBL kupitia Safari
Lager kwa kuandaa mashindano hayo, akisema kuwa serikali inatambua mchango wa
kampuni hiyo katika kujenga uchumi wa Taifa kupitia tukio hilo na mengineyo
kama mashindano ya Pool Safari Lager, Safari Wezesha na hata udhamini wao
katika michezo mbalimbali kama soka na mingineyo.
“Mashindano haya ni mazuri kwani yanawajengea
wateja wa nyama mazingira mazuri na salama katika kutoa huduma hii ya nyama
choma,” alisema.
Alizitaka baa ambazo hazikufika fainali,
kutokata tamaa na badala yake kujipanga kwa ajili ya mashindano ya mwakani, kwa
kurekebisha yale waliyokosea mwaka huu.
0 Comments