Social Icons

Monday, June 27, 2011

SHAGGY AZINDUA KWA KISHINDO TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2011,CCM KIRUMBA MWANZA

Msanii Shaggy aliwajibika Jukwaani kwenye uzinduzi rasmi wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2011.

Wapenzi wa burudani katika Jiji la Mwanza Rock City wamepata burudani ya aina yake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011 kutoka kwa mwanamuziki wa Kimataifa Shaggy mwenye asili ya Jamaica amabye pia amesema kuwa amekuja nchini akitokea nchini kwao Jamaica.

Shaggy amewapagawisha wapenzi wa burudani kwa nyimbo na mtindo wake wa kucheza ambao uliwafanya mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuchanganyikiwa kwa furaha kutokana na burudani ya mwanamuziki huyo.
Kwa upande wa wanamuziki wa hapa nchini wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama ‘Bongo Fleva’ ambao waliwapagawisha mashabiki katika tamasha ilo lililoaanza majira ya saa 6:05 mchana ni pamoja na Mwana FA pamoja na wanamuziki kutoka katika jumba la kukuza vipaji la THT akiwemo. Linah, Barnaba, Mataluma pamoja na Mwasiti.
Pindi walipopanda wanamuziki hao kwa nyakati tofauti mamia ya mashabiki waliojitokeza katika tamasha ilo walipagaawa kwa kupiga kilele za furaha kuonyesha hisia zao kwa wanamuzki hao.
Baada ya burudani kutoka kwa wanamuziki wa nyumbani ndipo ilipofika muda wa Shaggy kutoa burudani ambaye alipanda jukwaani majira ya saa 12:27 jioni akiwa na waimbaji wake watatu ambapo alianza kutoa burudani mfululizo kwa kupiga nyimbo zake zinazotamba na zile zilizowai kutamba miaka ya nyuma.
Baadhi ya nyimbo za zamani zilizowapagawasha mashabiki ni pamoja na wimbo wa ‘Angel’ ambao ndio uliokuwa wa kwanza kupigwa kwenye tamasha ilo.
Baada ya nyimbo hiyo zilifuata nyimbo nyingine zikiwemo ‘Strength for the Woman’, na ‘It wasn't Me’ ambazo ziliwahi kutamba na ziko kwenye chati hadi sasa .
Baada ya tamasha ilo la Mwanza burudani hiyo ya Serengeti Fiesta 2011 itafanyika tena mjini Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri na Shinyanga kwenye uwanja wa Kambarage Julai 2 mwaka huu.

Hapa Shaggy alikuwa akijitayarisha kupanda kwenye ngazi za Jukwaa CCM Kirumba.

Hawa ni waimbaji wake ambao walikuwa wakienda sambamba na Shaggy katika nyimbo zake zote, lakini majina yao hayakupatikana.

Imani , mimi Khadija na John Bukuku .

Hapa mwanamuziki Shaggy akilikaribia jukwaa kabla ya muda wake kutoa burudani akiwa na ulinzi.

Imani, Allan na mmoja ya wapiganaji wa SBL wakishangweka ndani ya CCM Kirumba Mwanza.

Mkuu wa Kitengo Cha Mambo ya Ndani Imani Lwinga na mmoja ya wapiganaji wa SBL wakiwa hawana Majotroo.

Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya Serengeti ambao ndiyo wadhamini wakuu wa tamasha hili Caroline Ndungu akiwa na Mwenyekiti wa Bodi SBL, Mark Bomani hapa wakifuatilia onyesho la mwanamuziki huyo wa Kimataifa.

Raha jipe mwenyewe hapa tukaamua kunesanesa baada kuguswa na moja ngoma zilizoachiwa na Shaggy.

Khadija Kalili, Mtangazaji wa Kipindi Cha XXL kinachorushwa hewani na Radio 88.4 Clouds FM B12 na Mtangazaji wa kipindi Cha Take One Zamaradi Mketema.


Baadhi ya wasanii wa miondoko ya Kizazi Kipya na kutoka Nyumba ya Kuibua Vipaji THT wakinesa na miondoko ya Shaggy.

No comments:

 
 
Blogger Templates