SERENGETI MACHIFU WA KISUKUMA WAMVISHA RUBEGA SHAGGY

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia Serengeti Mark Bomani akiwatangazia wakaazi wa Jiji la Mwanza hasa wazee wa Kabila la kisukuma waliojitokeza katika sherehe za Ekaristi Takatifu inayokwenda sambamba na sherehe za msimu wa mavuno Bogobogo ambapo leo Machifu wa Kisukuma walimpa baraka msanii huyo kwa kumkabidhi silaha za jadi tatu Usinga, Fimbo na kumvisha rubega jeusi.

Mkurugenzi Masoko wa Kamouni ya Bia ya Serengeti (SBL), Caroline Ndungu akiwa na msanii Shaggy katika viwanja vya Bujorwa.
Msanii wa Kimataifa Shaggy akiwa ndani ya Jumba la Makumbusho la Kabila la Wasukuma (SUKUMA MUSEUM).

Hapa Shaggy akitoka katika viwanja vya Bujorwa mara baada ya kupewa baraka na Machifu wa Kisukuma kaitka sherehe hiyo ya Ekaristi Takatifu ya Mavuno.

Shaggy Akisubiri kupewa baraka za wazee za kijadi kutoka katika kabila la Kisukuma.Msanii wa Kimataifa katika miondoko ya Dance Hall, Reggae Shaggy katikati akizunguma na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mlaika nje kidogo ya Jiji la Mwanza kushoto ni Meneja wa Bia ya Serengeti Allan Chonjo na kulia ni MKurugenzi wa Masoko SBL,Caroline Ndungu.


Shaggy akisindikizwa na vimwana wa Kisukuma mara baada ya kupewa baraka katika sherehe za Ekaristi Takatifu ya Mavuno.

Hapa vimwana wakijiweka tayari kumpokea Shaggy.

Akipata maelezo mafupi kuhusu sherehe hizo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Serengeti Mark Bomani.


Shaggy akiwa nje ya jengo la Makumbusho la Utamaduni na Historia ya kabila wasukuma.

Post a Comment

1 Comments

Anonymous said…
Dada Manji alipopewa Uchifu Yanga uliandika makala na kuelezea kwa urefu, je vipi kuhusu Shaggy? au sababu anatoka Marekani?

Mdau

Maryland