DHL WATOA VYANDARUA 1500 KITUO CHA KULELEA WATOTO SOS

Wafanyabiashara wanaojishughulisha na usafirishaji wa vifurushi na bidhaa mbalimbali DHL wametoa msaada wa vyandarua 1,500 leo kwa nyumba ya kulelea watoto yatima wanaoishi katika kituo cha (SOS Childrens Villages) kilichopo barabara ya Sam Nujoma Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa vyandarua hivyo Mkurugenzi Taifa wa Kijiji hicho cha SOS, Rita Kahurananga alisema kwa niaba ya kituo,watoto na uongozi wote wa SOS wanatoa shukrani za dhati kwa DHL.

Alisema msaada huo umekuwa ukiwa ni katika mpango mkakati wa kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria pia wakukuwa wakihitaji vyandarua hivyo msaada huo umekuja kwa wakati muafaka .

Kahuranaga aliendelea kwa kusema kuwa vyandarua hivyo watavigawa katika vituo vyao vungine vya kulelea watoto vilivyoko Mwanza, Arusha, Zanzibar, Bagamoyo, Shinyanga na Iringa.

Wakati huohuo aliongeza kwa kusema kuwa wanampango wa kuanzisha vituo vingine vya kulelea watoto katika kisiwa cha Pemba, Mtwara, Iringa na Mbeya ambapo pia wanahitaji wadhamini wajitokeza ili kufanikisha mpango huo endelevu.

Kituo cha SOS kiliasisiwa na Herman Gmeiner ambapo kituo cha kwanza alikilianzisha mwaka 1949 nchini Australia.
SOS ni shirika lisilo la kiserikali na wenye mipango ya muda mrefu ya kuweka malezi bora kwa watoto ambao huanza kulelewa kuanzia umri wa kuzaliwa hadi wanapopata umri mkubwa huku wengine wakimudu kujitengemea ambapo inalea watoto 419 katika vituo.
Mwisho.
Mtoto Kulwa akizunguma na mimi mara baada ya kukabidhiwa vyandarua hapa akirudi darasani.
Watoto Ahmed na Kulwa wakiwa na vyandarua ambapo pia waliwawakilisha wenzao.

Post a Comment

0 Comments