SERIKALI INAWAJIBU WA KUTENGENEZA MAZINGIRA RAFIKI KWA MTANZANIA

 

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo, akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 7 Agosti 2026 alipotembelea mabanda mbalimbali  ikiwamo Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara katika Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa 2026 yanayofanyika Viwanja vya Dkt. John Malecela Jijini Dodoma .

Amesema serikali inawajibu wa kumtengenezea mazingira rafiki Mtanzania ili kumurahisishia shughuli zake za kiuchumi.

“ Kila Mtanzania anapaswa kutengenezewa mazingira rafiki awe mkulima, mfugaji na mvuvi,” ameema Mhe. Londo.

Mhe. Londo amesema  kusema kuwa mwananchi anapopunguziwa gharama hizo anakuwa na uhakika wa kuzalisha kwa tija na kuwa na uhakika wa kuwa na akiba ya chakula cha kutosha.

Aidha, Naibu Waziri Londo alisema Serikali inachokifanya ni kujenga barabara, vivuko na madaraja ili kumuwezesha mkulima kutoka mashambani kwenda kwenye masoko na viwandani.

Alisema Serikali hivi sasa inaendelea kusambaza umeme kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) katika vijiji na vitongoji vyote ili kumpunguzia gharama mwananchi za uzalishaji.

Post a Comment

0 Comments