MEYA DKT. NICAS ASISITIZA  KUKAMILIKA UJENZI WA MATUNDU YA VYOO SHULE YA MSINGI TANDAU 


Mstahiki Meya wa Manispaa  ya Kibaha  Dkt.Mawazo Nicas  leo tarehe 5 Januari  2026 ameendelea na ziara yake  kwa kufanya ukaguzi  wa ujenzi wa matundu sita ya vyoo    katika Shule ya Msingi Tandau iliyopo Kongowe Wilayani kibaha Mkoani Pwani.

Akiwa katika ziara hiyo amesema kuwa ameridhishwa na hali ya ujenzi na kusisitiza   Afisa Utumishi kutoka fedha kiasi cha Mil.50 ili ujenzi huo ukamilike kabla ya Shule kufunguliwa  kwa sababu watoto zaidi ya 800 wanahitaji kutumia matundu ya vyoo hivyo 

"Nimeona hali ya ujenzi inaridhisha  hivyo  naamuru Afisa Utumishi aidhinishe kiasi cha fedha zilizobaki zije kutumika kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa hivi vyoo pamoja na kununua madawati na sitaki kuona mwanafunzi anakaa chini" amesema Dkt. Nicas. 

"Kamilisheni ujenzi wa matundu haya  harakauwezekanavyo ili pindi Shule zitakapofunguliwa  wanafunzi waweze kutumia kwa sababu uhitaji.ni mkubwa" amesema Dkt. Nicas.

Aidha Afisa Utumishi Manispaa  ya Kibaha Mrisho  Mlela amesema kuwa amepokea maelekezo na fedha  huzi zitatoka (kesho) tarehe 6 Januari  2026.

Akizungumza  na Waandishi wa Habari  Kaimu Afisa  Elimu Kata Julius  Samson amesema kuwa Shule  hiyo inakabiliwa na uhaba wa matundu ya vyoo na madawati.

" Natoa shukran  zangu za dhati kwa ziara  ya Mheshimiwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha  na namna alivyotoa atoa maelekezo kwamba fedha zitoke ili ziweze  kutatua kwa changamoto inayotukabili nasema asante  sana" amesema  Kaimu Afisa Elimu Kata  Julius. 

 Wakati huohuo  Dkt.Nicas amepokea malalamiko  ya kuomba kurejeshwa kwa gari la wagonjwa lililochukuliwa na Kituo Cha Afya Mkoani  huku akiongea kwa simumoja kwamoja na Mganga wa Kituo hicho ambaye amekiri kurudisha gari hilo mara moja.

Pia Dkt. Nicas amekagua ujenzi wa Kituo Cha Afya Kongowe ambapo amekagua upanuzi wa  majengo ya  majengo ya upasuaji ,wodi ya kuzalisha kina mama  na wodi ya watoto  njiti  zote zikiwa

katika hatua ya kukaribia kukamilika  pia amemsitiza Kamimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha  Mrisho Mlela kutoa  fedha kiasi cha Mi.50 ambazo zitasogeza ujenzi katika hatua fulani kwenye majengo hayo mapya .

Dkt.  Makidika amesema kuwa katika kituo hicho wamekuwa wakitoa huduma ya kuzalisha kwa dharura  tu na hadi sasa hawajawahi kupata  rekodi ya vifo vya wazazi .

" Hivi sasa  wajawazito hukazimika kutembea umbali wa Km 15 kufuata huduma ya uzazi ambapo  hulazimika kwenda Mkoani Kibaha au Mlandizi hivyo endapo pesa  itatoka kwa wakati itasaidia kukamilisha majengo hayo na kupunguza usumbufu kwa kina mama wanaojifungua" .

Dkt. Nicas ameahidi kuwa Manispaa itajitahidi  kumalizia majengo hayo .

" Nadhani  rukamilishe  haraka  ,tuone tunavyokwenda  kwenye bajeti tuipitishe  haraka ili majengo yakamilike tupeleke kicheko kwa qananchi" amesisitiza Dkt. Nicas .

Kadhalika  wakazi hao  wa Kongowe wameomba Manispaa  iwajengee soko kwa sababu hivi sasa wanakwenda kuhemea  soko  la Mlandizi, hoja hiyo imechukuliwa na utekelezaji  utafanyika.

Post a Comment

0 Comments