Mkurugenzi wa Kiduli FC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kiduli Security Ally Masimike amesema kuwa "awali ya yote anawapongeza wachezaji kwa kucheza mchezo mzuri na suala la kupoteza ni bahati mbaya hivyo wanakwenda kujipanga kuangalia wapi wamekosea ili watakapokuja kucheza katita fainali wanaimani matokeo yatakua mazuri.
"Leo tarehe 6 Januari 2026 tumecheza fainali ya kwanza na kupoteza lakini tunayo nafasi katika mechi ijayo tuna chukulia hii ni bahati mbaya tunakwenda kuziba upungufu"amesema Kiduli.

Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA) pia ni Msimamizi wa Michezo Mkoa kutoka Bodi ya Ligi Nasoro Shomvi 'Mbilinyi' ametoa wito kwa wadau wa michezo Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi katika fainali ligi darala la tatu ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza ambapo Bagamoyo Sugar ya Bagamoyo wamertoka kifua mbele kwa Kiduli FC ya Kibaha itakayo chezwa tarehe 12 Januari katika Uwanja wa Mwendapole, Kibaha.

Katika machine iliyochezwa jana tarehe 6 Januari 2026 Bagamoyo Sugar wametoka kifua mbele kwa kuongoza 1-0.
Mbilinyi amesema kuwa Ligi hiyo ilikuwa ni kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20.
"Timu ya Soka ya Bagamoyo ya imeifunga Kiduli Fc ya Kibaha kwa goli 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Tatu Mkoa wa Pwani ikiwa ni fainali ya kwanza" amesema Mbilinyi.
Mchezo huo umechezwa kwenye Uwanja wa Mwendapole Kibaha huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kupigwa Januari 12 kwenye Uwanja huo huo ikiwa ni fainali ya pili ili kupata bingwa wa Mkoa.
Bingwa wa Ligi hiyo atapata Kombe na atawakilisha Mkoa wa Pwani kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa.
"Mwaka huu katika fainali tutatoa Kombe kubwa kwa timu itakayoshinda pia kutakua na Mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Timu ya Baberian " amesema Mbilinyi.


0 Comments