POLISI PWANI YAJIVUNIA MAFANIKIO YA OPERESHENI NA MISAKO


Jeshi la Polisi  Mkoa wa Pwani  kwa kipindi  cha  miezi  mitatu kuanzia  Septemba  hadi Novemba 2025 ambapo wamefanya  misako ya  kuzuia  na  kutanzua  uhalifu  katika Wilaya  zote.

Akizungumza na Waandishi wa Habari  katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Pwani RPC Salim Morcas  amesema kuwa katika  operesheni  hizo  wamefanikiwa  kukamata  watuhumiwa 203  waliokutwa na makosa  mbalimbali.

" Katika  operesheni  na  misako  hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani  limekamata  Magobole 13 yaliyokuwa  yanamilikiwa  kinyume  cha sheria,Bastola  moja aina ya Luger M90 ikiwa na risasi tisa, Bunduki aina  ya  Shortgun  moja , mitambo mitatu ya  kupikia   pombe  ya moshi  na pombe ya moshi  lita 375" amesema Morcase.

Aidha  amesema kuwa Jeshi hilo wamekamata  dawa za kulevya aina ya bhangi  viroba  21, debe tano , puli 557 kete 3998, misokoto 193,pakiti 43  za bhangi aina ya skanka vyote vikiwa  na jumla  ya kilogramu328.5 pia wameteketeza mashamba  ya bhangi  yenye ukubwa  wa hekari4,Mirungi  bunda  187 zenye  jumla  ya kilograms  187.

RPC Morcase amesema kuwa pia  wamekamata Gari  aina ya Scania  lenye namba  za usajili T.625 CBD na trela  lenye namba  T.467 lililobeba  shehena  ya nondo mali inayodhaniwa kuwa ya wizi.

Amesema kuwa  katika operesheni  hizo  Jeshi la Polisi limefanikiwa  kuokoa  mali mbalimbali ambazo ni  Pikipiki 37 za aina tofauti,  Simu za Mkononi 93  za aina mbalimbali,  Laptop moja  na CPU moja,Bomba  28za Umeme, Ng'ombe  39, madumu 12 ya mafuta  ya Dizel@20,mifuko 100 ya Saruji,Luninga tano za aina mbalimbali,vifaa mbalimbali  vya nyumbani , magodoro mawili ,viatu jozi  sita,vipande  vitatu vya vitenge,vipande vitatu vya Khanga.

Vitu vingine vilivyokamatwa ni Madumu 206 ya mafuta ya kula  aina ya Korie@lita 20,Mitungi ya gesi  15 ya aina mbalimbali, Radio nane , Sabufa  na Spika zake na vipande 16 vya nyama ya pori.


Kamanda Morcase  amesema kuwa  katika  makosa  yaliyoripotiwa  kwenye vituo vya Polisi, jumla ya kesi 47 zimefikishwa Mahakamani  na kupata ushindi kwa  huku watuhumiwa 53 wamehukumiwa vifungo mbalimbali  Mahakamani ikiwemo vifungo vya maisha kwa makosa ya kubaka na kulawiti.

Wakati huohuo amesema kuwa  Jeshi hilo limetoa Elimu ya Usalama  barabarani ambapo Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limekamata jumla  ya makosa 74,446 na  kulipiwa  faini  za za papo kwa papo kiasi  cha Shilingi 2,233,380,000
.

Aidha  elimu  hiyo  ya usalama barabarani  imetolewa  katika Shule  za  Msingi 42,Shule za Sekondari 36 ,Vyuo vya Udereva viwili ambapo jumla ya wanafunzi 3234  wamepata elimu hiyo. 

"Madereva  na abiria  katika stendi na vijiwe 54 vya bodaboda wamefundishwa  matumizi  sahihi  ya alama  za barabarani, haki na wajibu  wa abiria  na watembea  kwa miguu huku jumla ya madereva  38 wamefungiwa leseni zao kwa  makosa  mbalimbali  ya usalaam barabarani"  amesema RPC Morcase. 

" Jeshi la Polisi  Mkoa wa Pwani  linatoa  rai  kwa wananchi  kuendelea  kulinda  amani  na utulivu  kwa kufuata  sheria  na kanuni  za nchi  aidha katika kuelekea  sikukuu za  mwisho  wa mwaka  linawakumbusha  wananchi  wanaotarajia  kusafiri kwenda  Mikoa mbalimbali  kwa kutumia  vyombo vya moto  na kuzingatia  sheria  za usalama  barabarani  na kutumia  madereva  wazoefu ili kuepusha  ajali zinazoweza kuepukika na kusisitiza  abiria kutosimama na wakishikwa mshtakiwa wa kwanz atakuwa abiria  aliyesimama

Post a Comment

0 Comments