DKT.NICAS: MIGOGORO YA ARDHI KIBAHA SASA BASI


 Dkt.Nicas Mawazo Meya wa Manispaa ya Kibaha 

Mstahiki Meya wa kwanza Manispaa ya Kibaha Dkt. Nicas Mawazo ameapa kuwa atavalia njuga migogoro ya ardhi ndani ya Manispaa ya Kibaha iliyopo Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.

Dkt. Nicas amesema hayo leo mara baada ya kula kiapo cha kuwa Meya wa Manispaa alipozungumza na Waandishi wa Habari na kusema atalivalia njuga suala la migogoro ya ardhi pamoja na kero zingine mbalimbali 

Aidha Dkt. Nicas amesema kuwa anatoa rai kwa Wakuu wa Idara mbalimbali na Watendaji wake ndani ya Manispaa hi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na amewataka wawe wachapakazi na kuhudumia wananchi

 Wakati huohuo amewasisitiza Madiwani wa Manispaa ya Kibaha ambao wamekula kiapo leo tarehe 4 Desemba 2025 kuwa waadilifu na kutanguliza maslahi ya wananchi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku

Baada ya kuchaguliwa Dkt. ameongoza kikao cha mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Kibaha huku Naibu Meya ni Aziza Mruma na wengine walioteuliwa ni pamoja na Wenyeviti na wajumbe wa Kamati za kudumu

" Tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo, mimi nitakuwa sauti ya wanyonge wasio na sauti ambapo nimepanga kila Jumanne na Alhamisi nitakuwa na ratiba ya kusikiliza kero za wananchi,” amesema Dkt Nicas.

“Tumepewa dhamana ya kuwatumikia wasio na sauti mimi nahitaji kazi tu, sitaki rushwa,” amesema Nicas.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini, Mwl. Mwajuma Nyamka, amewasihi Madiwani na Watendaji kuwa wamoja, kuonesha upendo na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu yao.

Nyamka amesema kuwa makundi yote yafe na kuacha yaliyopita na kujenga ya sasa na yajayo kwani kipaumbela kikubwa ni kuhakikisha miradi mbalimbali inatekelezeka na kukamilika kwa wakati " amesema Nyamka.


 

Post a Comment

0 Comments