Na Mwandishi Wetu.
Baada ya Tanzania kutajwa na mtandao wa World Travel Awards kama nchi inayoongoza kwa Utalii wa Safari mwaka 2025 imekuwa ni chachu ya kutangaza mazao mapya ya Utalii katika soko la Dunia yanayopatikana ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi anayeshughulikia huduma za utalii ambaye yupo Bahrain ambapo hafla ya utoaji wa tuzo za WTA zimeanyika amesema Ngorongoro ona nafasi kubwa kimataifa kuuza mazao mapya ya utalii duniani kutokana na kukua kwa sekta ya utalii.
Tanzania imetunukiwa tuzo hiyo adhimu katika sekta ya utalii duniani wakati wa hafla ya 32 ya World Travel Awards (WTA) iliyofanyika katika ukumbi wa Exhibition World Centre nchini Bahrain tarehe 6 Desemba, 2025 .
Akizungumza baada ya Hafla hiyo Kamishna Kobelo ameeleza kuwa kufuatia ushindani wa tuzo za utalii katika nyanja mbalimbali Tanzania hususan eneo la hifadhi ya Ngorongoro itaendelea kuboresha miundombinu ya utalii na kutangaza mazao mapya ya utalii hasa utalii wa Makumbusho Jiopaki ya Ngorongoro Lengai na Olduvai pamoja na vivutio vya urithi wa utamaduni na mambo kale ili yafahamike zaidi na kuweza kushindanishwa kidunia.
Kobelo ameeleza kuwa Tanzania ni sehemu salama na ina vivutiio vingi ambavyo vinapaswa kupelekwa soko la Kimataifa na kuendelea kupokea wageni wengi na pato la Taifa kuongezeka ili kuendeleza matokeo chanya ya Filamu ya Tanzania the Royal tour na Amaizing Tanzania.
Nchi ya Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa tuzo za utalii duniani mwaka 2026 ambapo wadau wa Sekta ya Utalii kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni watashiriki





0 Comments