CCM: TATIZO SIYO UCHAGUZI WALA DEMOKRASIA


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kwa kile kinachopitiwa na Tanzania wakati huu hakikuanza jana, juzi au mwezi uliopita bali ni mapambano ya kiuchumi baada ya ardhi yake kugundulika madini adimu duniani.

CCM kimesema huenda wakajitokeza maadui zaidi watakaotumiwa kama njia ya kufanikisha mkakati wa kuhatarishaa amani endapo WaTanzania watagawanyika. 

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar , Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis ameyaasa mataifa makubwa yaache kutoa visingizio vya kudhoofu kwa demokrasia au kutaja chaguzi kuu hazikuwa huru ili kutimiza matakwa yao.

Mbeto alisema Duniani kumeibuka vita ya kiuchumi iliojaa hila na ghilba zitokanazo na uchu wa kuhodhi madini adimu yanayohitajiwa kwa Maendeleo ya mataifa makubwa.

Alisesma hadithi au simulizi za kuipa majina mabaya Tanzania na vitisho zilianza kwa kudai kuna uongozi wa kidikteta, ukandamizaji haki, dermokrasia, uhuru wa vyombo vya habari na kilichoitwa kifo cha upinzani.

"Hizi zote ni hadithi za ubabaifu, miradi miiwili ya Urani eneo la Mkuju na Liganga imefumua joto la taharuki duniani. Wakati Mkuju si mgodi tu wala Urani bali pia ni mojawapo ya maeneo muhimu duniani" alisema Mbeto.

Alisema hatua ya Shirika la Nyuklia la Urusi kuchukua mradi wa nyuklia ndio mwanzo wa kuzuka fitna nyeusi baada ya Tanzania na Urusi kuzindua Kiwanda cha majaribio cha usindikaji wa Uranium Mkuju.

Alisema kwa Mradi wa Lindi Liganga kampuni za Magharibi toka Mwaka 2018–2023 zilijadiliana bila mafanikio huku China, Falme za Kiarabu na kampuni ya Gazprom ya Urusi, zikionyesha nia ya kuanza kushiriki.

 "Taswira iliopo ni Uranium kwenda Urusi Gesi itahodhiwa na China, Nchi za ghuba, Urusi huku nchi za Magharibi zikitaka kujua endapo hakutakuwa na mabadiliko yoyote " alieleza.

Mbeto alisema hapo ndipo ilipoanza vita ya kidijitali kwani kama inavyojulikana siku hizi vita haipiganwi kwa bunduki bali kwa matumizi ya mitandao ya kijamii.

"Tanzania haitapuuza msimamo wake wa kujadiliana na kiungwana ili kufikia makubaliano ya kiungwana" alisema.

Post a Comment

0 Comments