Na Mwandishi Wetu Morogoro
Mchezo wa riadha umeonesha kuwa ni zao muhimu la michezo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kutokana wanariadha wa mchezo huo kutoka Ngorongoro kuzoa jumla ya medali saba (07) pamoja na ushindi wa mbio za kupokezana vijiti.
Timu ya Ngorongoro ya riadha ilinogesha mashindano hayo kwa wakimbiaji wake kuonesha vipaji vya hali ya juu na kuendelea kudhirisha kuwa Ngorongoro ni Premium Safari Destination.
Katika salamu zake kwa wanamichezo wote wa Ngorongoro Kamishna wa Mamlaka hiyo Bwana Abdul-Razaq Badru amewapongeza kutokana na kushiriki kwao kwenye michezo na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro pamoja na kudumisha nidhamu na uwajibikaji wakati wote wa mashindano hayo.





0 Comments