PUNZI:JENISTA MHAGAMA AMEACHA ALAMA KWA VIJANA

Aliyekua Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama 

Na Omari Punzi , Kihaba

"Nenda mama nenda pumzika  salama hakika kazi kubwa umeifanya kwa vijana wa Tanzania " 

Mimi mwanao kwa kazi kubwa uliyoifanya kwa vijana ukiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu. 


Nakumbuka ulivyocheza ule mpira kama pele na kulazimisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 🇹🇿 kukubali na kupitisha sheria ya kuanzishwa kwa Baraza la Vijana Taifa na kumbuka ulisimama kidete sheria ikawekwa ya namba 12 mwaka 2015.

Ukasimama mpaka sheria hiyo ikatangazwa katika gazeti la serikali namba 348 la tarehe 15 Septemba 2017.

Ulitamani kuona Vijana wakijengwa kuwa wazalendo.

Ulitamani kuwa vijana wawe na Baraza lao ambalo litaeleza hisia zao Baraza hilo halitofungamana na Taasisi au Chama chochote.

Ulisimama kidete kuhakikisha sheria inatungwa maana tangu 1980 ilikuwa ni kilio cha kila siku

Mimi mwanao nakupa pongezi hata kuanzishwa kwa Wizara ya Vijana ni sehemu ya hisia zako wewe ni Mzalendo


Nenda mama nenda hakika safari ni ya wote 

Mimi mwanao nakuombea Dua upumzike Salama

Post a Comment

0 Comments