Na Mwandishi wetu.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kuwajengea uwezo watumishi wake kwa kuwapa mafunzo ya namna bora ya kusimamia masuala ya Itifaki na kuhudumia wageni mbalimbali wanaotembelea hifadhi hiyo.
Kaimu Meneja Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka hiyo Hamis Dambaya amesema kuwa kufanyika kwa mafunzo hayo yeye na timu yake kutasaidia kuwajengea uwezo watumishi wa kitengo hicho katika kipindi hiki ambacho mamlaka hiyo imedhamiria kufanya mabadiliko makubwa kiutendaji na kihuduma
Akifungua mafunzo kwa Maafisa Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka hiyo jijini Mwanza Mshauri wa Jeshi la Uhifadhi Ngorongoro Kanali Fikiri Machibya ameeleza kuwa ni muhimu kwa kwa maafisa uhusiano kwa umma wa mamlaka hiyo kuendelea kujiimarisha katika masuala ya mawasiliano na itifaki za kijeshi ili kuimarisha utendaji kazi wao na kufikia viwango ambavyo mamkala imejiwekea kwenye mipango yake.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kuwa kivutio bora barani Afrika kutokana na umahiri wake katika kusimamia shughuli zote za uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii jambo ambalo limekuwa likivutia wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo.




0 Comments