JWTZ , POLISI WAPONGEZWA KWA KUIMARISHA ULINZI KIBAHA 9 DESEMBA


Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi Wilayani Mkoani Pwani wamepongezwa kutokana na kuimarisha ulinzi siku ya kumbukumbu ya sherehe za Uhuru wa Tanzania iliyoadhimishwa tarehe 9 Desemba 2025 ambapo ilikuwa siku ya mapumziko nchi nzima.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo tarehe 12 Desemba 2025 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Mwalimu Mwajuma Nyamka amesema kuwa uamuzi wa kutokuwa na sherehe zinazoambatana na gwaride siyo geni kwani ilishawahi kutokea katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano iliyokuwa chini ya Hayati Rais John Pombe Magufuli. 

"Ikumbukwe kwamba pindi alipingia madarakani 2015 alitangaza kughairi kufanyika kwa sherehe za kumbukumbu ya sherehe ya kuoata uhuru na fedha zilikwenda kutumika katika miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara ya Bagamoyo" amesema Nyamka.
 
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Kibaha Elina Mgonja ameongeza kwa kusema kuwa wakaazi wa Kibaha wanatoa shukrani kwa majeshi hayo kutoleta taharuki na kuonekana kutoa maelekezo kwa njia rafiki kwa wale ambao walilazimika kutoka kwa sababu maalumu.

"Watanzania tumemuomba Mungu atuepushe na mabalaa na ametenda hili ni jambo la kushkuru na kikubwa zaidi tumeilinda amani yetu na iendelee kuwa hivi ,tumesherehekea kwa amani na utulivu binafsi nimesherehekea siku yangu ya kuzaliwa siku hiyo kwa amani" amesema Mgonja. 

"Ni jambo la kushkuru kwamba tumekaamajumbani mwetu na kusherehekea kwa amani na utulivu asante sana majeshi yetu, tunamuomba Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kumpa moyo pia tunamuambia kwamba mamlaka yoyote inawekwa na Mungu na siyo mwanadamu" amesema Mgonja.

Ameongeza kwa kusema kuwa wananchi wote wapenda amani wamemuomba Mungu awaaibishe wale wote waliokuwa na nia ovu na kweli wameaibika Mungu ibariki Tanzania.

Post a Comment

0 Comments