MBETO: HAKUNA MHINDI ASILI YAKE MAKUNDUCHI


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Kulingana na historia, hakuna watu jamii ya wahindi ambao asili yao Afrika isipokuwa wazazi wao walihamia na kuzaliana na wengine wanatambulika kuwa ni raia wa nchi hizo huko walikozaliwa.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Mafunzo, Itikadi na Uenezi, Khamis Mbeto Khamis akizungumza hivi karibuni kuhusiana na kauli za kibaguzi, zinazodaiwa kutolewa mara kwa mara na viongozi wa ACT Wazalendo, alisema hakuna mhindi ambaye asili yake Makunduchi, Zanzibar.
Mbeto alionyesha kushangazwa na Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Ismail Jussa Ladhu kujinasibu kuwa asili yake Makunduchi huku akimnyooshea kidole Dkt. Hussein Mwinyi kuwa ni mgeni Zanzibar.
“Mhindi gani kwao Makunduchi? Umemuona wapi mhindi Afrika” wote wamehamia hivyo ACT kuwaweka watu katika matabaka ni ubaguzi usio na maana kwani visiwa vyote ulimwenguni watu wanahamia kama ilivyotokea Zanzibar.
“Unaweka tabaka, ukisema mtu fulani mgeni kwa kuwa ametoka sehemu mojawapo ya mwambao wa Tanzania Bara, sio sahihi, sababu Zanzibar ni Cosmopolitans “watu wenye asili mchanganyiko” alisema Mbeto.
Mwenezi huyo, anakumbusha historia kwa kueleza kuwa Zanzibar ni ya namna yake na ya kipekee Afrika Mashariki na watu wa kwanza kufika Zanzibar ilikuwa karne ya kwanza kutoka mwambao wa Bara kuanzia Lamu, Mombasa hadi Msumbiji.
Alibainisha kuwa kunako karne ya pili na tatu ikafika misafara ya Washihiri kutoka Yemen na baadae Shiraz kutoka nchi za Syria na Iran (Persia) na Waarab kutoka Oman.
“Wakati wote huo wa mwingiliano, watu walikuwa wakiendelea na shughuli zao za maisha kama kawaida na Zanzibar imetawaliwa na Ureno kwa miaka mia mbili” alisema.
Alibainisha kuwa Waarab, wamekaa Zanzibar kwa zaidi ya miaka 100 na wapo mpaka waChina ambao ni waZanzibar hivyo akataka jamii iwakatae wanaohubiri ubaguzi.
Alisema Zanzibar kuna mpaka Wahindi na mmojawapo ni Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Ismail Jussa Ladhu ambaye wazazi wake walitokea, India na kuishi Zanzibar.
“Othman Masoud Othman mgombea nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia ACT Wazalendo, wazazi wake asili yao Mafia, mkoa wa Pwani Tanzania Bara” nani anashughulika nae?” alihoji.
Alisema, chama hicho kimeishiwa sera, hawana la kuwaambia WaZanzibari ndio maana wamebaki kwenye ubaguzi, Muungano na chuki binafsi.
Alibainisha kuwa Mzee Marehemu Ali Hussein Mwinyi, alitokea Mkuranga, mkoa wa Pwani akahamia Zanzibar akiwa mdogo, akasoma na kaoa Zanzibar kama ilivyokuwa kwa wazazi wa Jussa.
“Kasoma na kaoa Zanzibar, mama yake Dkt. Hussein kazaliwa Bumbwini, Mbilimbini na Makoba, Misufini kote kwao” alisema na kuongeza kuwa kwa aliyoyafanya Dkt. Mwinyi Zanzibar, CCM haina shaka na ushindi wake 29 Oktoba mwaka huu.
Alisema Dkt. Mwinyi hakuna ambako hakugusi kwenye Ilani na ndio maana kampeni zake ni za kuwaonyesha alichofanya, anachomalizia na kile anachotaka kufanya kwa ajili ya Zanzibar 2025/2030.

Post a Comment

0 Comments