Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, amemkabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo), Mhe. Luhaga Joelson Mpina.
Tukio hilo limefanyika leo, Ijumaa Agosti 15, 2025, katika ofisi za Tume, ambapo Mgombea huyo aliambatana na Mgombea Mwenza wake, Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej. Tume inatarajia kufanya uteuzi wa wagombea Agosti 27 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mwambegele, alikumbusha wagombea wote kufuata masharti na taratibu za uchaguzi, huku akisisitiza umuhimu wa kampeni za kistaarabu na zenye kuzingatia sheria.
Shughuli hiyo iliudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ACT Wazalendo pamoja na wanachama wa chama hicho waliokusanyika ukumbini kushuhudia tukio hilo.




0 Comments