MGOMBEA KITI CHA UBUNGE KIBAHA MJINI SILVESTRY KOKA ARUDIISHA FOMU

Mgombea wa kiti cha Ubunge kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Silvestry Koka amerudisha fomu  ya kuwania  kiti cha Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini  Mkoani Pwani leo  tarehe 27 Agosti, 2025.

Koka akizungumza  na wananchi  mara baada ya kurudisha fomu yake katika ofisi za Tume ya Uchaguzi  zilizopo  Manispaa ya Kibaha amesema kuwa  "fomu zimepolewa  na kwa sasa najipanga kwa uchaguzi ujao wa 2025" amesema .

"Sasa najipanga kwa kampeni za uchaguzi  nawasisitiza kama jinsi tulivyoongea  siku nilipochukua fomu kwamba kule tulikotoka tulikua tunafanya mazoezi ya kukimbia  na kumpata mkimbiaji bora ambaye ni mimi hivyo tofauti na makundi yafe chama kwanza mtu baadaye"amesema Koka.
"Tofauti zetu tumezimaliza makundi yasiwepo tena kundi ni moja tu ambalo ni CCM, tuungane kwa pamoja tukazitafute kura  za wananchi popote walipo ili Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika Oktoba 29 ,2025" amesema.

Mbunge Koka amesema wananchi Jimbo la Kibaha wahakikishe  wamamchagua mkimbiaji namba moja  Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge  na Madiwani  wote wa Kata 14 wanapata kura za kutosha  ili kutumiza mafiga matatu.

Post a Comment

0 Comments