Leo katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Dodoma, nikiambatana na Mgombea Mwenza, Balozi Ndugu Emmanuel John Nchimbi, niliporejesha fomu za uteuzi wa kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Ninawashukuru sana wanachama wa chama chetu Chama cha Mapinduzi (CCM), waliowawakilisha mamilioni ya wanachama wenzetu kutoka kila mkoa nchini, kwa kuniunga mkono katika fomu za udhamini. Tunapoelekea kuzindua kampeni za uchaguzi, tuendelee kudumisha umoja huu ili kukihakikishia chama chetu ushindi, na kwa idhni ya Mwenyezi Mungu turejee kuendelea kuwatumikia wananchi kama yalivyo matarajio yao.
Serikali yaendelea kuimarisha usalama dhidi ya majanga nchini
-
*Na Mwandishi wetu- MBEYA*
*Mkurugenzi msaidizi wa Kituo cha Taifa cha Operesheni na Mawasiliano ya
Dharura kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratib...
1 hour ago




0 Comments