DKT. DIMWA AWAFUNDA VIONGOZI WA CCM SHULE YA MWALIMU NYERERE

Naibu Katibu  Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dkt.  Mohamed Said Dimwa  amewaasa wanachama wa Chama hicho kuepuka makundi ya uhasama, uzandii wakisiasa na udhaifu katika maamuzi wakati wa kuelekea  katika kipindi cha uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika Oktoba 2025.

"Chama chetu cha CCM  kimejiimarisha  kwa kuwa na mikakati ya kisayansi na madhubuti  ya kuhakikisha  tunapata ushindi na kudumu dhidi ya hila na mbinu za wapinzani ambao lengo lao ni kuturudisha nyuma"

amesema Dkt.Dimwa.

Naibu Katibu Mkuu  CCM  Zanzibar Dkt.Dimwa amesema hayo alipokua mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo  kwa viongozi wa chama yanayoendelea  katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Kwa Mfipa Mkoani Pwani  yameanza Juni 6 hadi 12.

Dkt.Dimwa ameendelea kwa kusema kuwa  anawakumbusha viongozi hao ambao wako kwenye mafunzo kuwa wanajukumu la kwenda kutoa  maelekezo  ya chama kwa watendaji ikiwa ni pamoja na Jumuiya zote za CCM  sambamba na kutii miongozi na maagizo ya chama ,kusimamia  utekelezaji  kwa vitendo, kuheshimu  vikao vya katiba  na kujenga  nidhamu binafsi sambamba na  kutekeleza  maamuzi yote ya chama.

"Nawaagiza nendeni mkaendeleze  mpango wa kushuka hadi kwenye matawi ili kuongeza wanachama nankuhimiza uwajibikaji ulipaji wa ada za chama, kushiriki  kikamilifu katika  maandalizi ya uchaguzi ujao utakaofanyika Oktoba 2025.

"Nawasisitiza  nendeni mkaimarishe  chama na jumuiya zake zote  ikiwa ni pamoja na kuandaa  mpango kazi  wa kina  kwq ufuatiliaji  wa shughuli za chama  na kutoa maelekezo  ambayo mlahakikishe kuwa yanatekelezwa" amesema Dkt.Dimwa.

Dkt. Dimwa amesema kuwa viongozi hao ambao wako kwenye mafunzo wanatakiwa kuwa  daraja  la mawasiliano  linalofikisha  utekelezaji  wa maagizo  ya chama hadi ngazi ya chini.

"Urafiki wetu baina ya CCM na CPC  umependelea kuimarika  kwa kupitia  misaada  ya  kifedha , kitaaluma na kiufundi  ikiwa ni pamoja na kufadhili kwa ukarimu  mafunzo kama haya kwa wanachama na viongozi wa CCM. 

CPC imewakilishwa na Mkufunzi Yao Jianguo  atashirikiana na Naibu Mkurugenzi  wa Kituo Cha  Mabadilishano  ya Kimataifa CPC-CIE  Xu Sujian pia watashirikiana na timu ya wawakilishi wa CPC nchini Tanzania


 Aidha Dkt. Dimwa amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan amemwagiza amwaeleze kuwa wakawe mabalozi wa matumaini , maendeleo na mshikamano kwa wananchi wote hasa katia kipindi hiki muhimu tunapokaribia uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025.

"Ndugu wana mafunzo nimejulishwa kuwa mtakuwa na ma 17 zilizochaguliwa kwa umakini mkubwa ili kuwajengea uwezo wa hali ya juu wa Uongozi kimkakati na kiitikadi nawakumbusha kuwa dhima kubwa ya mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wa kiutendaji wa chama kwa ajili ya zoezi kubwa la uchaguzi mkuu ujao.

Napenda kutoa shukran za dhati kwa Chama Cha Kikomunisti Cha nchini China CPC kwa kuendelea kudumisha udugu,ushirikiano wa kihistoria na mshikamano wa kweli baina ya vyama vyetu na mataifa yetu.

Post a Comment

0 Comments