ZLATAN IBRAHIMOVIC AJIVINJARI SERENGETI


 Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Sweden, Zlatan Ibrahimovic, ametua nchini nakuuchapisha picha akiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.

Ujio wa @iamzlatanibrahimovic , ambaye amewahi kuzichezea klabu kubwa Ulaya zikiwemo @manchesterunited @fcbarcelona, @acmilan @juventus @inter unatajwa kuwa kichocheo kikubwa kwa sekta ya utalii nchini, hasa ikizingatiwa kuwa akaunti yake ya Instagram ina wafuasi takribani milioni 63 duniani.

Tanzania imeendelea kujitokeza kama kitovu cha utalii katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, huku watu mashuhuri kutoka maeneo mbalimbali duniani, wakiwemo wanamichezo, wakizidi kuitembelea nchi hii maarufu kwa vivutio vyake vya asili.

Kwa sasa, idadi ya watalii wanaoitembelea Tanzania imeongezeka na kufikia takriban milioni tano kwa mwaka, mafanikio ambayo yanachangiwa na juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, katika kutangaza vivutio vya utalii kupitia njia mbalimbali za ubunifu.


Mojawapo ya jitihada hizo ni ushiriki wake katika filamu maarufu ya The Royal Tour, iliyomwonyesha @samia_suluhu_hassan akieleza uzuri wa vivutio vya Tanzania, hatua iliyosaidia kuitangaza nchi kimataifa na kuongeza mvuto wa utalii

Post a Comment

0 Comments