MWANDISHI WA GAZETI LA Habari LEO AULA TFF

Mwandishi wa  habari za michezo wa gazeti la  HabariLEO Rahel Pallangyo amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutoka Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Tanga leo.

Katika uchaguzi huo Rahel alimwangusha Allanus Lwena aliyekuwa anatetea nafasi yake. 

Kwa upande wa Mwenyekiti amechaguliwa Emanuel Chaula na wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa ni Maulid Mwikalo na Jovin Ndimbo. 

Mwenyekiti Chaula amemteua Michael Kassanga kuwa Makamu Mwenyekiti  pia anatakiwa  kuteua   wajumbe watano watakaoingia kwenye Kamati ya Utendaji.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Wakili George Banoba ametoa rai kwa  viongozi wapya kwenda kufanya kazi kufuata muongozo  na katiba ya FRAT. 

"Mliochaguliwa wote mmeapishwa kulinda katiba na miongozo ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT), FRAT na TFF hivyo katekelezeni majukumu yenu" amesema Wakili Banoba.

Naye Mwenyekiti Emanuel Chaula amewashukuru wajumbe kwa kumchagua na kuwaahidi kuwatumikia.

Post a Comment

0 Comments