CAG MSTAAFU UTOUH ATOA USHAURI OFISI YA MSAJILI HAZINA

Mdhibiti   na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu CAG Ludovick Utouh  ameishauri  serikali  kupitia  Ofisi ya Msajili wa Hazina  kutengeneza  timu maalumu ya wataalamu  itakayofanya  uchambuzi yakinifu kwa Mashirika  ya Umma na taasisi za serikali ambayo  hayajiendeshi kwa faida na kuleta hasara kwa nchi.

 "Kwa miaka mitatu mfululizo sasa serikali tumekua tunafanya vizuri sana katika makusanyo yetu ya mapato  lakini utakuta kule kuzidisha mapato hakujatokana na bidii zetu za kuongeza mapato yetu ya ndani isipokuwa imekuwa na kukopa zaidi ya  tulivyopanga CAG anatuambia kwamba kuna mabilioni yalikua yakusanywe na wahusika lakini hayajakusanywa hivyo zile pesa tunazozikusanya tuzisimamie  na kuzitumia  vizuri zaidi" amesema 

CAG Mstaafu Utouh.

 Amesema kuwa timu hiyo maalumu itakayoundwa itapaswa  kuaangalia kiini  kinachosababisha hasara kwa mashirika hayo  pia wafanye mapitio katika sheria  zilizopo ikiwa pamoja na  sheria ya manunuzi ya umma.

"Ipo haja ya kutengeneza sheria  ya kuimarisha ofisi ya  mkaguzi wa ndani  na kuangalia utendaji wake  ofisi hii bado changa kwani  imeanzishwa mwaka  2012 ila ina umuhimu mkubwa,

waweze kupata tarifa za utendaji wa serikali kabla ya ripoti ya CAG kutokelewa".

"Hali tuliyonayo sasa hivi fedha na rasilimali za nchi siyo za mtu  bali ni pesa za wananchi, serikali imepewa mamlaka ya kukusanya hizo pesa kikatiba

"Hivi karibuni tumeona kwenye ripoti ya CAG serikali imefanya vizuri katika hesabu za serikali asilimia 95 za tasisi za serikali zimefanya vizuri.

Maafisa masuhuli wanafanya manunuzi bila kupata uhakiki kwa mwanasheria mkuu wa serikali, hivyo vinakua ni viashiria vya uhakika wa rushwa kuna haja ya watu wanaoteuliwa kwenye nafasi za uongozi wawe na uzalendo na kuthamini pesa za umma na kabla hujaitumia ifikirie kama pesa hiyo ingekuwa ya kwako je usingeithamini amesema CAG mstaafu Utouh.

CAG Mstaafu Utouh  amesema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tano yanayoendelea  katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kwamfipa Wilayani Kibaha Mkoani Pwani   kwa Viongozi wa umma kutoka katika taasisi na mashirika mbalimbali nchini.

Wakati  huohuo  Mkuu wa Shule   ya Uongozi ya Mwalimu  Nyerere Profesa Marcelina Chojoriga  amesema mafunzo hayo  yamelenga  kuwajengea uwezo  washiriki hao 40  na kuwakumbusha majukumu yao  ya kusimamia  kwa weledi  Mashirika ya umma na taasisi za serikali.

"Kiongozi ndiyo mbeba dira na maono  hivyo viongozi lazima awe msimamizi mzuri  na mwenye  weledi ili aweze kuleta  tija pia ni mbeba maonona  dira ya  kuwaendeleza wale anaowasimamia katika eneo lake".

"Wote tumeona na kusikia ripoti ya CAG  lazima tukubaliane katika ushirikishwaji wa wananchi viongozi wawashirikishe katika mipango ya  maendeleo  kwani ni haki ya mwananchi  kushirikishwa, sheria ya serikali ya mtaa inasema kila mwananchi mwenye umri wa mika 18 anatakiwa kushiriki katika mipango  ya maendeleo na kufuatilia utekelezaji wake  hasa katika maendeleo   na mipango ya serikali  hivyo kila kiongozi atambue kuwajibika katika hilo"

Baadhi ya Taasisi hizo ni Stamico,TTCL,
TAMISEMI ,
Wizara ya Maji,TBA ,Youth Development, TARI ,TACAIDS,TBC,BIOTEC Kibaha Mji ,TANESCO, PCCBna Ocean Road.

Post a Comment

0 Comments