ALHAD MUSSA AMEKATAZA KUTOHUKUMU NAFSI ZA WATU

Mwenyekiti  Kamati ya Taifa ya Maridhiano  nchini Sheikh  Alhad Mussa ameiasa jamii kuacha tabia ya kuhukumu mtu , hakuna kifo kibaya kama mtu kuondoka ghafla  unakwenda 'fresh'bila kuomba toba kwa mola wako  lakini  muumini yeyote anayeumwa kwa muda mrefu hupata muda wa kutubu na kurejea kwa mola wake.

Alhad Mussa amesema hayo  tarehe 21 Aprili  2025 alipokua akitoa mawaidha kwa waombolezaji waliofika  Bunju nyumbani kwa aliyekua Mkurugenzi wa  Kampuni ya Lino International Agency marehemu Hashim Lundenga 'Uncle Hashim' ambapo mwili wake umesafikishwa na kuzikwa leo  tarehe 23 Aprili 2025 Kidatu    Mkoani Morogoro.

"Tuache tabia za kutoa hukumu kwa wenzetu pindi wanapotangulia mbele ya  haki kwa sababu mandiko matakatifu ndani ya Qur ani tukufu yanasema kuwa kuumwa ni ibada hivyo mtu anapoumwa kwa muda mrefu Mwenyeezi Mungu humsafisha madhambi yake na pia hupata muda wa kutubu kadhalika ifahamike kwamba hakuna dhambi kubwa ama isiyosameheka mbele ya Mwenyeezi Mungu na hakuna anayejua mja anapoomba toba kwa muumba wake hiyo siri ya baina ya wao wawili" amesema Alhad Mussa.

"Uislamu ni dini ya mazingatio na fikra  mwanaadamu anatakiwa awe na mazingatio katika mambo makubwa hasa kifo , tumekua tukiwasindikiza ndugu zetu lakini tunakosa mazingatio ya kifo na kusahau kuwa  kila aliyezaliwa na mwanamke hata akiishi maisha mazuri na marefu kiasi gani iko siku atakufa" .
"Kifo kina kata ladha ya kila kitu , mkeo,mumeo, watoto na mali zako vyote utaviacha na utaondoka maiti huwa vinamfuata vitu vitatu viwili hua vinarudi ambavyo  ni ndugu  , na jamaa  watoto na  mali zake vitarudi na wala hakuna ndugu au mtoto atasema nizikwe naye ila kinachobaki pale ni amali njema , matendo mema je mahusiano yako na Mungu yakoje unaishije na wenzako , je unaabudu Mungu pamoja na neema za pumzi na afya na kunshukuru Mungu kwa kumuabudu ? jihesabuni nafsi zenu kabla hamjahesabiwa je una shukrani za pumzi  na mali alizokujaalia Mungu? 

Ishi na watu wote kwa tabia nzuri bila kujali dini, sisi wanadamu tunapoishi tunapitia mambo mengi sana mwanadamu kutenda dhambi ndiyo ubinaadamu na waliobora kwa binaadamu ni kwa wale wanaotubia.
Mwenyeezi Mungu hatuonei taabu tunapotenda dhambi ila baada ya dhambi tubia , Mwenyeezi Mungu anawapenda wenyekutubia  dhambi zao na kujitwaharisha na kukiwa na mtu hapa hajatenda dhambi basi huyo ni Malaika sababu wao hawamuasi Mwenyeezi Mungu siku zote wanafanya yale mema  waliyoamrishwa na Mungu.
"Mlango wa toba uko wazi huo ndiyo ukumbusho na tuwe tunatoa faraja maana kuna viongozi  huwa wanatoa mawaidha makali usiwakatie tamaa waja wa Mwenyeezi Mungu milango ya pepo iko wazi wewe unawafungia milango ya peponi kama pepo ya babaako  na toba kati ya mola na mja wake  Mwenyeezi Mungu anasemsa rehema zake zimeenea kwenye kilakitu" amesema  Alhad Mussa. 
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Ephraim Mafuru  akimuelezea marehemu Lundenga  amesema kuwa ataendelea kumkumbuka  kutokana na nguvu yake ya ushawishi siyo tu kwa wasichana warembo bali hata kwa wadhamini katika Kampuni mbalimbali  ambapo alikuwa na nguvu ya kutoa ushawishi na kuweza kupata udhamini mnono kwa kuanzia ngazi ya vitongoji hadi taifa.
Meneja wa zamani wakinywaji cha Pilsner Ice  waliowahi kutoa udhamini mnono katika shindano la Miss Tanzania David Minja amesema kuwa "wote tunajua pengo ambalo tasnia ya ulimbwende  imepata na  alama kubwa ambayo Lundenga ameiacha  kwa taifa japo hakufanya mwenyewe alikuwa na jopo la watu wengi nyuma yake pamoja na warembo walioshiriki ,kwangu mimi tasnia ya urembo ilikua ni ngazi  ya kuwajenga kina mama shupavu  na viongozi bora katika jamii hilo liko wazi hivyo itoshe kusema apumzike kwa amani na tuendelee kumuezi" amesema  Minja.

Akizungumza  na kutoa salamu za pole kwa niaba ya warembo wote waliopita katika jukwaa la  la Miss Tanzania  Faraja Kotta Nyarandu (Miss Tanzania 2001)amesema kuwa "Anko Hashim Lundenga amegusa wanawake wengi  kwa kupitia yeye tumeweza kuvumbua vipaji mbalimbali kwa kuwa jukwaa la Miss Tanzania lilikua ni tanuri kwa walimbwende nchini Lundenga alikua baba mlezi, rafiki na kama kiongozi ambaye amegusa  maisha ya warembo nchini ambapo wameweza kutimiza njozi zao katika maisha" amesema Faraja.

"Miss Tanzania ni tanuru lililotupa chachu kwa kila mmoja wetu na  katika kumbukumbu ya kila mwanamke  ambaye alipita kwenye jukwaa la Miss Tanzania amesimama imara katika eneo lake"amesisitiza Faraja .
Mh.Balozi wa Tanzania  nchini Sweden Mobhare Matinyi  akisaini kitabu cha maombolezo  nyumbani  kwa marehemu Lundenga  Bunju Jijini Dar  es Salaam. 
Mwili wa marehemu  Lundenga  ukiwasili nyumbani kwake Bunju  Jijini Dares Salaam jana tarehe 21 Aprili 2025 .
Baadhi  ya warembo walioshiriki shindano la ulimbwende la Miss Tanzania katika miaka tofauti  wakiwa waliofika msibani wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwili wa marehemu  Anko Hashim Lundenga  ukisaliwa Salat jeneza kijijini kwao kabla ya mazishi yaliyofanyika  leo  tarehe 22 Aprili 2025 Kidatu  Mkoani Morogoro.
Hakika sisi ni wa Mwenyeezi Mungu na kwake tutarejea (Innalilah Wainna Ilaih Rajioun).

Post a Comment

0 Comments