RAS PWANI AFUNGUA KONGAMANO LA VIJANA KUHUSU UMUHIMU WA UZINDUZI MWENGE WA UHURU

Katibu Tawala Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Skauti Mkuu wa Tanzania  Rashidi Mchatta amefungua Kongamano  la siku mbili lililojikita katika kutoa elimu juu ya umuhimu wa uzinduzi  na mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa  Bertil Merlin na kuwakutanisha wanafunzi wa Kibaha Sekondari, Chuo Cha Afya na Sayansi Tumbi.

 Mchatta amesema kuwa Kongamano  

" Nawashukuru waandaji na washiriki wa Kongamano hili muhimu la vijana kuhusu umuhimu wa kushiriki Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 ambalo litafanyika siku mbili leo tarehe 28  hadi  29 Machi 2025."

"Serikali inatambua umuhimu wa kundi la vijana katika kuleta mageuzi ya Kijamii na Kiuchumi kutokana na ari, nguvu na ubunifu walionao. Kwa kutambua hilo serikali kwa kushirikiana na wadau imekuwa ikitoa kipaumbele kwa vijana kupata elimu na makuzi bora, kuwapa fursa ya kupata mikopo ya asilimia 10 kupitia Halmashauri na Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (Build Better Tomorrow – BBT) " amesema  RAS  Mchatta. 

Amesema  Kongamano hili limeandaliwa katika mtazamo wa kuwajengea uwezo vijana juu ya umuhimu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika kujenga udugu, utu, uzalendo, uwajibikaji katika usimamizi wa shughuli za maendeleo na kutambua fursa za kiuchumi.

"Nimeambiwa kuwa mada zitakazojadiliwa kwa siku mbili ni kama zifuatazo:- 

Historia na Falsafa ya Mwenge wa Uhuru Uzalendo, Itifaki na Maadili

Fursa za Kiuchumi zinazotokana na Mwenge wa Uhuru

Umuhimu wa kushiriki katika shughuli za utunzaji wa nazingira

Umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025

stadi za maisha na stadi za kazi

malezi na makuzi kwa vijana

afya na afya ya uzazi

Sambamba na mada hizo itatolewa  elimu ya matumizi sahihi ya  Mitandao ya simu na elimu  ya utunzaji wa fedha katika Taasisi za kifedha.

" Nawasihi vijana kusikiliza kwa makini na kutafakari mada hizo ili ziweze kuleta mabadiliko chanya kimtazamo katika maisha yenu binafsi, kijamii na maendeleo ya nchi yetu" amesema RAS Mchatta. 

Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 utazinduliwa Mkoa wa Pwani kitendo ambacho kinaonesha nia njema ya dhahiri Rais  Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan  kuendeleza na kuenzi kwa vitendo yale yote aliyoturithisha baba wa taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage.

Tarehe 2 Aprili 2025 Mbio za Mwenge wa Uhuru zitazinduliwa katika viwanja vya Shirika  la Elimu Kibaha Mkoani Pwani ambapo mgeni  Rasmi atakuwa Makamu wa Rais  Dkt. Philip Isdor Mpango.

Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 ni ‘Jitokeze  Kushiriki Uchaguzi  Mkuu  Wa Mwaka  2025 Kwa Amani na Utulivu'.

"Rai yangu kwenu mjitokeze kushiriki katika Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa namna ambavyo mtaelekezwa na viongozi katika maeneo mnayoishi" amesema Mchatta.

 "Tukifanya hivyo tutaupata ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa ufasaha ili muweze kushuhudia kwa vitendo yale yote mtakayojifunza katika Kongamano hili" amesema Mchatta.

Meneja wa  Benki ya NMB Tawi la Mlandizi. William Marwa mesema kuwa Benki ya NMB  wamechangia kiasi cha Mil.30 ikiwa ni katika kufanikisha   Uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru utakaofanyika  Aprili 2 ,2025  kwenye Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha Mkoani  Pwani  ambapo  wahudhuriaji 16,000  wanatajiwa kushuhudia uzinduzi huo.

Baadhi ya wadau waliojitokeza kushiriki katika  ongamano hilo ambalo  litahitimishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani  Alhaji Abubakari Kunenge.
Wanafunzi wa Sekondari  ya Kibaha  wakifuatilia mjadala kwa makini  kwenye Kongamano  hilo.

Post a Comment

0 Comments