MAANDALIZI UZINDUZI MBIO ZA MWENGE WA UHURU UMEFIKA 96%

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amesema kuwa maandalizi ya uzinduzi wa kuwasha Mwenge  wa Uhuru umefikia asilimia 96.

RC Kunenge amesema hayo leo tarehe 25 Machi 2025 alipozungumza na Waandishi  wa Habari  na kusema kuwa zimebaki shughuli ndogondogo.

"Tunategemea kupata wahudhuriaji 16,000.

Kama jinsi mnavyoona Uwanja umependeza tumeotesha majani na kutengeneza majukwaa manne ikiwa ni pamoja na jukwaa la VIP katika 

Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha  Tumbi Pwani. 

RC Kunenge amesema kuwa mambo yanazidi kwenda kama vile yalivyopangwa, uzinduzi  na  Uwashwaji wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa utafanyika tarehe 2 Aprili 2025.

"Tumetengeneza miundombinu ya maji , umeme na pia tumeweka taa ambazo zitatumika hata baada ya sherehe za kuzindua kuwasha Mwenge wa Uhuru uwanja utatumika kwa shughuli mbalimbali.

Wakati huohuo ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani na mikoa jirani wanashiriki katika uzinduzi huo kikamilifu ili waweze kujionea yale yatakayifanyika siku hiyo.

"Kauli mbiu ya Mwenge wa uhuru mwaka huu inasema "Jitokeze kushiriki uchaguzi Mkuu 2025 kwa amani na utulivu" amesema Kunenge.

Post a Comment

0 Comments