KEDS YATOA ZAWADI YA SIKU YA WANAWAKE JIRANI NA KIWANDA

Mkurugenzi wa Kiwanda Cha Keds Tanzania Limited  Chen akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya kina mama waliofika kupokea zawadi ya Siku ya wanawake Duniani kwenye tukio lililofanyika leo tarehe 13 Machi 2025,Kibaha Mkoani  Pwani.

Katika  muendelezo  kusherehekea Maadhimisho ya Sikukuu ya Wanawake Duniani Kiwanda Cha Keds Tanzania Limited kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani  Pwani kimetoa zawadi ya bidhaa zinazozalishwa Kiwandani hapo kwa Wanawake wanaoishi maeneo ya kuzunguka kiwanda hicho.

Akizungumza mara baada ya kutoa zawadi hizo za sabuni ya unga 15 na za miche katoni 10 kwa kina mama 89 wanaoishi  katika eneo jirani na Kiwanda hicho kilichopo Kata ya Picha yandege Kibaha mkoani Pwani..

Mkurugenzi wa Kiwanda Cha Keds Tanzania Limited  Bob Chen  amesema   kuwa wametoa zawadi hizo kwa kina mama ikiwa ni katika kuwatakia kila lenye kheri wanawake wote  na kuahidi kutoa ushirikiano kwa wakazi hao utakapohitajika.

Cheng amesema kuwa wamewapatia misaada hiyo ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wa wanawake ambao ni mkubwa katika kuleta maendeleo kwenye jamii.

"Kiwanda kinaungana na wanawake katika maadhimisho haya hivyo tumeona turudishe kwa jamii ikiwa ni katika ushirikiano na wananchi katika kuleta maendeleo,"amesema Cheng.

Amesema kuwa kiwanda kitaendelea kushirikiana na jamii katika masuala mbalimbali ya maendeleo hususani kwa wananchi walio jirani na kiwanda na wananchi wote kwa ujumla.

Meneja wa Keds Michael Mbaraka Lugalela  amesema kuwa utaratibu huo  wa  kutoa  zawadi kwa wananchi  utakuwa endelevu kwa jamii.

Bi Mary Mkwizu na Jasmini Issa  wakiwa wamebeba zawadi zao.
Baashi ya kina mama ambao ni wakaazi  katika eneo la Lulanzi Kata ya Pichayandege  Kibaha ,Pwani wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kupokea zawadi   zao ambazo ni  sabuni ya unga n amiche kutoka Kiwanda cha Keds Limited. 

Mary Said  ambaye amewawakilisha mabinti katika kupokea zawadi hiyo amesema anatoa shukran  kwa Kiwanda hicho  kwa kuwakumbuka kwa mara nyingine  na kwamba  hii inakuwa mara ya pili kwake kupokea zawadi  na kuwataka waendelee kujali wananchi kama jinsi wanavyofanya tangy Kiwana hicho kilipoanzishwa.

Naye Meri Mkwizu amesema kuwa sabuni ni muhimu sana kwa familia na ni moja ya vitu muhimu katika mahitaji kwenye familia na hutumika muda wote.

Mkwizu amesema kuwa sabuni ina bajeti kubwa kutokana na matumizi yake ikiwa ni pamoja na kufulia nguo, kuoshea vyombo, kuogea na kufanyia usafi wa aina mbalimbali ambapo jumla ya wanawake 89 walipewa zawadi hizo

Akishukuru kwa msaada huo wa sabuni za unga na vipande Jasmini Issa amesema kuwa wanashukuru kwa zawadi hiyo kwani itawasaidia katika matumizi yao ya kila siku.

Issa amesema kuwa zawadi hiyo imeonesha jinsi Kiwanda hicho cha Keds kinavyoshirikiana na jamii katika suala zima la maendeleo ambapo wamekuwa wakisaidia miradi mbalimbali inayohusu wananchi katika eneo hilo.

Post a Comment

0 Comments