RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KUZINDUA JNHPP RUFIJI MKOANI PWANI AGOSTI 22 ,2026


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema maaandalizi ya uzinduzi wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere lililopo Wilaya Rufiji yamekamilika.

Akizungumza leo tarehe 20 Agosti 2026 katika mkutano na Waandishi wa Habari amesema kama ambavyo mmeona kwenye Vyombo vya Habari serikali kupitia Waziri wa Nisahati lakini na Msemaji Mkuu wa Serikali wametoa taarifa ya tukio kubwa la kihistoria la uzinduzi wa Bwana la kuzalisha umeme la Rufiji Hydro Project (JNHPP) utakao fanyika Rufiji tarehe 22 Agosti 2026.

RC Kunenge amesema tunatarajia mgeni rasmi katika uzinduzi atakuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini pia tutakuwa na wageni wengine kutoka katika mikoa mbalimbali watakaokuja katika Mkoa wetu pamoja na wageni kutoka nje ya nchi yetu.

"Uzinduzi huu unatimiza ndoto ya Watanzania inatimiza ndoto ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere na nchi yetu imekuwa na dhamira ya kujitosheleza kwa umeme ikibidi hata kusaidia jirani zetu muda mrefu" amesema RC Pwani.
Ameongeza kwa kusema kuwa tukio hili ni la kihistoria niwaombe wakaazi wa Mkoa wa Pwani kamakawaida yetu tuoneshe ukarimu ambao ni utamaduni wetu.

RC Kunenge amewataka wakaazi Mkoani hapa kujitokeza katika uzinduzi rasmi wa Bwawa la Kufua Umemel aMwalimu Julius Nyerere Wilayani Rufiji .


Amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi atuq itakayofungua fursa za kibiashara kwa Mkoa wa Pwani kutokana na kuwa na uhakika wa huduma bora ya umeme.

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi mdogo ofisini kwake amesema kuwa mradi huo wa JNHPP ambao asilimia 60 upo Mkoani Pwani na asilimia 40 upo katika Mkoa wa Morogoro. 

Aidha amewapongea wananchi wa Mkoa wa Pwani kwa kuendelea kutunza vyanzo vya maji na mazingira vilivyopo.

Safari ya kuelekea uzinduzi wa Kituo Kikubwa Zaidi cha Uzalishaji Umeme wa Maji Afrika Mashariki imefika ukingoni. Huu ni mradi wa kihistoria unaoendelea kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya sekta ya nishati nchini Tanzania. 

Post a Comment

0 Comments