WAKONGO WAGOMA KUZIKA BINTI YAO


pichani  ni marehemu Berliss Mujinga enzi za uhai wake.
Wakati huohuo  babamdogo wa marehemu  Mchungaji Enock  Ambroseo amesema kuwa   marehemu  Berliss na baba yake wameingia nchini  kwa miezi mitatu  wakitokea Lubumbashi  nchini Congo. 

"Baada ya kutoa taarifa  kwenye Jumuia ya Watu wa Congo  tumeaamua kuwa na msimamo mmoja kwamba hatutakwenda kuchukua kibali cha mazishi ya binti yetu hadi pale uchunguzi utakapokamilika ili marehemu  apate stahiki zake kwa kukatishiwa uhai"amesema  Ambroseo.
Pichani  ni baba wa marehemu Mchungaji  Kalanba Mukala Louis  ambaye ni muumini wa Kanisa la Pentecoste makaazi wa eneo la Mkuza Mharakani Picha ya Ndege Wilayani Kibaha Mkoani Pwani. 

Kibaha ,Pwani

Raia wenye asili ya Jamhuri  ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo (DRC) wanaoishi nchini  wameweka msimamo wao wa kugoma kuzika mwili wa binti Mujinga Ngalula   Berliss (17) ambaye mwili wake uliokotwa hivi karibuni  maeneo ya pori  la Msangani Wilayani Kibaha Mkoani Pwani akiwa amefariki kwa 

kuchomwa ni kitu chenye ncha kali shingoni mwake kama jinsi ilivyoelezwa na Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Pwani  Muhudhwari Msuya  kwenye taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari.

Akizungumza na Waandishi  wa Habari  nyumbani kwake leo tarehe 26  Oktoba ,2024 eneo la Mkuza  Muharakani  baba wa marehemu aliyejitambulisha kuwa ameingia nchini akitokea Lumbumbashi  mahsusi kwa kutoa huduma katika Kanisa la dhehebu la Pentecoste Mchungaji Kalanba Mukala Louis amesema Jumatatu  iliyopita  marehemu alimuaga  mdogo wake mwenye umri wa miaka 11 kuwa anakwenda saluni kusuka nywele  na baada ya hapo hakurudi nyumbani waka kupata taarifa zozote .

"Tulimtafuta sana bika mafanikio hadi usiku nikowa n babake mdogo bila mafanikio 
 nilimtuma mdogo wake aende  kumuulizia kwa  majirani  wote hawakufahamu alipokwenda  nikatoa taarifa kwa Mwenyekiti  wa Mtaa tukashirikiana kusambaza picha zake kwa majirani na wachungaji mbalimbali  siku ya Jumatano Mwenyekiti  alinipigia simu na kuniambia amepata taarifa kuna mwili umeokotwa  mapori ya Msangani uko Hospitali ya Rufaa Tumbi Mkoa wa Pwani hivyo  tukaongozana kwenda kuuangalia nilipofika chumba cha maiti nikamtambua mtoto wangu lakini nikazuiwa nisimguse kwa sababu za kiusalama niliuona mwili wa mwanangu ukiwa  umerowa damu huku akiwa ametobolewa macho nimelia sana"  amesema Mchungaji  Louis   ambaye ni  baba wa marehemu Berliss. 
   Baadhi  ya  waombolezaji  wakiwa msibani.
Alidha aliyekua Mwenyekiti wa Umoja wa Wakongomani wanaoishi nchini  Abdallah  Serge amesema  kwa niaba ya Umoja wao wamegoma kumzika marehemu Berliss mpaka watakapo ridhika na uchunguzi wa mauaji  hayo tofauti na ilivyo sasa  hawajaridhika na taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani.

"Jana usiku  nimempigia simu Balozi wetu wa Congo  amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha binti yetu na amesema ataandika barua kwa Wizara ya Mambo ya Nje kutoa malalamiko  yao na kuiomba serikali ya Tanzania iweze kutoa taarifa zitakazowaridhisha ndipo ikiwemo gharama za kumstiri marehemu " amesema Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wakongomani  wanaoishi nchini.


Akizungumza  kwa njia ya simu Kaimu Kamanda  wa Mkoa wa Pwani Muhudhwari Msuya  amesema  uchunguzi wa kuwabaini wahusika bado unaendelea

Post a Comment

0 Comments