UWEKEZAJI SEKTA YA MASHIRIKA YA UMMA UMEFIKIA TRILIONI 86

 
Kibaha, Pwani 

Mkurugenzi wa 
Uwekezaji Ofisi ya Msajili  Hazina  Lightness Mauki  amesema uwekezaji wa serikali katika mashirika ya umma nchini umefikia shilingi trioni 86 kufikia mwaka 2024 hivyo amewataka Viongozi wa mashirika ya umma kuhamasisha wananchi wanapata tija kwa uwekezaji huo.

Amesema hayo wakati akifunga Mafunzo kwa viongozi wa Taasisi na Mashirika ya umma nchini walioshiriki mafunzo ya 23 ya Uongozi katika shule ya uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere kwa Mfipa Kibaha Mkoani Pwani akimwakilisha Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu.

Amesema katika mwaka 2023 uwekezaji huo katika Mashirika ya umma umefikia shilingi trioni 64 na kufanya ongezeko la uwekezaji wa shilingi trioni 32 mwaka huu ambao unahitaji umakini mkubwa katika usimamizi ili kuutekeleza katika kuhudumia wananchi.

Amesema viongozi hao wa mashirika ya umma wanatakiwa kuelewa kuwa wao ndiyo chachu ya taifa kubadilika na kufikia malengo yake ya mabadiliko ya kiuchumi kama dunia inavyobadilika na kupiga hatua za maendeleo.

"Sasa kama tunazungumzia uwekezaji huo wa shilingi trioni 86 hivyo na wasimamizi wa mapato ni vema tukajipanga katika kuhakikisha tunasimamia uwekezaji wetu huo mzuri ili ulete tija kwa wananchi amesema Lightness.

Mauki ametaja uwekezaji huo wa fedha ambao serikali imewekeza kuwa upo katika sekta ya zote ikiwa ni pamoja na sekta ya Maji, kilimo, madini na masoko ya fedha.

Aidha amewataka viongozi hao wa mashirika ya umma kujipanga kusimamia uwekezaji huo mkubwa katika nchi ili ulete tija kwa taifa.

"Ni mimi na wewe ndiyo wakuhakikisha wananchi wanapata tija ya kunufaika katika uwekezaji huo mkubwa wa shilingi trioni 86" amesema Lightness.

Malengo ya serikali  ni kupunguza hali ya utegemezi wa Mashirika ya  Umma  kwa serkali  nawapa changamoto  tunapotoka hapa twende tukawe  chachu ya mabadiliko katika Taasisi tunazo zisimamia.

"Tunapaswa kwenda sambamba  na falsafa ya Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan ya  mabadiliko  hivyo tuanze kubadilika sasa ili kuleta matokeo chanya" amesema Lightness.

Viongozi  hao wamehitimu mafunzo ya Uongozi na Menejimenti kwa viongozi wa  Mashirika ya Umma ambayo yamefanyika kwa muda wa siku tano.

"Tunawategemea ninyi ili mkawe chachu  ya maendeleo  kwenye Taasisi  zenu  mnazotoka kila mmoja kwa sababu mmepata fursa hii adhimu  katika  maeneo muhimu  hivyo nendeni mkaitumie  ipasavyo elimu mliyopata hapa  kwa sababu sisi hatuishi kwenye kisiwa  twende   sambamba  na mabadiliko ya kiuchumi  sambamba  na teknolojia.

"Hivi sasa tumeona kuna mabadiliko  ya  ya teknolojia  ikiwa pamoja na akili mnemba hivyo twende nayo sambamba  kama jinsi serikali  yetu imeona  mabadiliko ni jambo muhimu  katika nyanja zote  hivyo viongozi wote kwa pamoja  twendeni tukaishi haya mabadiliko  na sisi pia tubadilike" amesema  Lightness.

Amesema kuwa Mashirika ya Umma yamekua chachu  ya mabadiliko ya uchumi nchini na ni vema tujipange kusimamia uwekezaji. 

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Shule ya Mwalimu Nyerere Prof. Marcelina Chijoriga amsema kuwa wahitimu hao wakiwa kwenye mafunzo yao pia wamesoma somo la uzalendo na kusisitiza  kuwa kila Mtanzania anatakiwa asome somo hilo  pamoja na somo la Usalama wa Taifa kwa sababu  viongozi  hao ambao wanapokea miradi mingi na kukutana na mambo mbalibali hivyo suala la usalama wa taifa Bi  muhimu zaidi katika kujenga uchumi.

"Tumejaribu kuwaambia wanapaswa kuwa na mahusiano  mazuri na wadau  wanaofanya nao kazi kwani inawezekana  ukawa Mkurugenzi  Mtendaji  mzuri lakini pale linapokuja suala la kujieleza wengi hushindwa ni imani yetu mara baada ya mafunzo haya  watakuwa wameiva kiutendaji kwenye  nyanja zote.
Prof. Chijoriga amesema kuwa  katika shule hiyo wanatoa mafunzo kwa viongozi mbalimbali na kwa upande wa Taasisi za Umma wamelenga kuwabadilisha viongozi wake kutokana na umuhimu wake wengi mmeona baadhi ya mashirika yamekufa na mengine hayafanyi vizuri.

Amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwabadilisha viongozi hao wa umma ili walete ufanisi katika utendaji kazi wao.

Chijoriga amesema kuwa viongozi wa taasisi na mashirika ya umma endapo hawatapata mafunzo hawataweza kuboresha utendaji kazi wao hasa ikizingatiwa kuna mambo mbalibali yanabadilika hivyo nao waendane na hali halisi
Naye Mwenyekiti wa Wahitimu Simion Marwa amesema kupitia mafunzo hayo, wamejifunza nyenzo mbalimbali za kiutendaji kwa maslahi ya Taifa na bara zima la Afrika kwa ujumla, Ulinzi wa Taifa na Umajumui. Tumejifunza jinsi harakati za ukombozi na mikakati iliyotumika kufikia malengo ya ukombozi.
Tumejifunza jinsi uongozi na usimamizi wa kimkakati katika mageuzi ya kiuchumi na kijamii unavyoweza kuongeza ufanisi wa taasisi zetu. Ili kuongeza tija na ufanisi, mipango ya kimkakati lazima ieleweke kwa kipindi husika. Tunapotafuta fursa ni lazima kutanguliza maslahi ya Taifa."

"Vile vile maarifa tuliyopata katika uendeshaji wa mashirika yalenge kwenye ubunifu, uwajibikaji, uaminifu, nguvu ya pamoja katika utendaji, usawa, uwazi na uhuru katika uongozi wa kimkakati" Amesema Marwa.

Post a Comment

0 Comments