Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Daniel Chongolo (Mb) amesema kuwa Mkoa wa Pwani utaanza kilimo cha mbogamboga na matunda kitakachoanza hivi karibuni katika eneo lenye ukubwa wa eka 200 .
Akizungumza leo tarehe 16 Machi 2026 wakati akikagua eneo hilo lililopo Ruvu Stesheni Kibaha Vijijini Mkoani Pwani amesema kuwa ameridhishwa na mandhari hayo na kusisitiza kuwa kilimo hicho cha mbogamboga na matunda kitazalisha ajira kwa vijana wa Wilaya ya Kibaha na Dar es Salaam pamoja na wananchi wanaoishi katika maeneo ya jirani .
"Mahitaji ya mbogamboga na matunda ni makubwa hivyo shamba hili litasimamiwa na wataalamu wetu ambao wataelekeza walimaji kilimo cha kisasa ili kiwe chenye ufanisi na kuleta tija ambapo Kibaha itaillisha Dar es Salaam na Zanzibar kwa matunda na mbogamboga" amesema Mhe.Chongolo.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema kuwa hiki kitakuwa killimo cha muda mfupi na chenye tija kwa jamii ambapo
leo tumekuja kufanya tathmini ya eneo hili ambalo kilimo kitafanyika kisasa na kitakuwa cha kipindi cha mwaka mzima bila kutegemea mvua sababu tunayo miundombinu ya kumwagilia maji safi na eneo hili litaanza kusafishwa mara moja ikiwa ni katika hatua za awali za kuandaa shamba kwa kufuata maelekezo kutoka kwa wataalamu wetu





0 Comments