RAS PWANI AITA MASHABIKI KWENDA KUIPA HAMASA TIMU YA KIKAPU JKT


Kutoka kushoto ni Afisa Michezo Mkoa wa Pwani Grace Bureta ,Katibu Tawala Mkoa wa Pwani ambaye alikua mgeni rasmi  na Katibu wa TOC ,Filbert Bayi wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Urunani BBC ya Burundi. 
Kutoka Kushoto ni Afisa Michezo Mkoa wa Pwani Grace Bureta ,Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Rashidi Mchatta  na Katibu wa TOC Meja Mstaafu Filbert Bayi  ambaye ndiye mmiliki wa Uwanja wa Ndani ambao michuano hiyo inaendelea wakiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya JKT.
Baadhi ya Maafisa wa timu ya JKT wakifuatilia mchezo huo.
Katibu wa Chama Cha Riadha Tanzania (TOC) Filbert Bayi  akiteta jambo na  Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Rashidi Mchatta  kwenye Uwanja wa Ndani  wa Filbert Bayi  kwenye michuano hiyo ya Kikapu Zone Five .
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani  Rashidi Mchatta ametoa wito  kwa  wakaazi wa Mkoa wa Pwani  na Mikoa ya jirani kujitokeza kwenda  kushuhudia michuano ya kikapu kufuzu klabu bingwa Afrika (BAL) kanda ya Mashariki  inayochezwa Uwanja wa ndani wa Filbert  Bayi  uliopo Mkuza Kibaha .
RAS Mchatta amesema hayo  jana usiku mara baada ya kushuhudia  timu ya JKT   lipokipiga na timu ya Urunani kutoka Burundi ambao wageni hao wamemaliza mechi hiyo kwa kushinda kwa vikapu 83-60.
Aidha, RAS Mchatta  aliyekuwa mgeni rasmi katika michuano hiyo,  ametoa  wito kwa wakaazi wa Mikoa ya Pwani na Dar e s Salaam kujitokeza kwenda kuangalia mechi zinazo endelea na kutoa hamasa kwa timu ya JKT  ambao wanawakilisha nchi.

"Wananchi waje kutoa hamasa pia kuna jambo la kujifunza kwenye michuano hii nimeangalia nimeona kuna wachezaji wengi wa Kimataifa na mchuano ni mkali" amesema  RAS Mchatta.
Rais wa Chama Cha Mpira wa Kikapu Tanzania ( TBF)  Michael  Kadebe amesema  kuwa michuano  hiyo inashirikisha nchi  tano ambazo ni JKT  ambao ndiyo Mwenyeji , Urunani BBC (Burundi), Beau Vallon Heart (Seychelles), Nairobi City Thunder (Kenya) na GNBC kutoka Madagascar. 
Aidha jioni ya leo JKT watashuka tena dimbani kukiputa na timu ya GBNC ya Madagascar. 
Michuano  hiyo  imezinduliwa  jana tarehe 16 Oktoba  hadi 20 Oktoba  2024.

Post a Comment

0 Comments