KITUO CHA OLYMPAFRICA KIBAHA ,PWANI WAANDAA MAFUZO KWA WAALIMU 30 WA JUDO

Hapa mafunzo kwa vitendo yakendelea kwenye Uwanja wa Ndani wa Kituo Cha Olympafrica Wilayani Kibaha Mkoani Pwani. 
Wakati huohuo Katibu Mkuu wa TOC  na Meja Mstaafu  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Filbert Bayi amesema mafunzo hayo yameandaliwa na Kamati ya TOC ikiwa ni  katika mwendelezo  wa mafunzo mbalimbali wanayoyaandaa pia  amesisitiza  kwa kusema kuwa kufuatia kukwama kwa vifaa vya Judo Bandarini suala hilo liko nje ya uwezo wa TOC, huku akivitaka vyama kutumia anuani za serikali  ili kukwepa changamoto za kulipa ushuru "Hayo magodoro  ya mchezo wa Judo hiyo ndiyo kama    nyasi bandia kwa mchezo wa soka ambazo serikali  imetoa msamaha wa  ushuru hali ambayo imechangia ukuaji wa mchezo wa soka ," naiomba serikali ifikirie kutoa ushuru  kwenye vifaa vyote vya michezo nchini ambavyo huagizwa kutoka nje ya nchi na kuweza kunusuru na kukuza vipaji vya michezo  ukowemo Judo" amesema  Bayi.
 
Kuhusu faida ya mafunzo haya kwa  Makocha wa Judo  amesema kuwa  endapo kila Kocha atafundisha  wachezaji  wawili watakua wamepata wachezaji 60 katika mchezo wa Judo ambao ni muhimu katika maisha, nimesoma kitabu kimoja kinaeleza  kuwa  Rais  wa Urusi ni  bingwa  wa  Judo  hii ni  ninaimani  kwa sababu ya ulinzi wake binafsi"
amesema Bayi.
Waalimu 30  wa Mchezo wa Judo  kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar  wakiwa katika picha ya pamoja na  Mkufuzi UWW Erdal Dogan ambaye ni raia wa Uturuki. 

Aidha Makocha hao wa mchezo wa Judo wameanza mafunzo ya siku kumi ambayo yameanza leo 22, Septemba,2024  katika Kituo Cha  Olympafrica  Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

Katibu  Mkuu Chama  Cha Mchezo wa Judo Tanzania  Innocent John Mallya amesema kuwa  mafunzo yameanza leo 22Septemba   hadi Oktoba mosi 2024 ambapo waalimu wa Judo nchini  watapatiwa mafunzo  na Mkufunzi UWW Erdal Dogan ambaye ni raia wa Uturuki.

Katibu Mkuu wa Judo nchini Mallya amesema kuwa hali ya mchezo wa Judo inaridhisha kwa sababu wametoka kushiriki katika michuano ya Olympic  iliyofanyika Jijini Paris na kushika nafasi ya 16 bora.
 
 Kuhusu changamoto  wanazokabiliana nazo katika mchezo huo amesema kuwa ni  ukosefu wa vifaa vya kuwafundisha watoto kuanzia umri wa miaka saba na kuendelea.

"Mchezo  huu wa Judo  una ukosefu vifaa kwani hata hawa waalimu wanaofundishwa watakapo maliza mafunzo yao kitakacho wakwamisha ni  uhaba wa vifaa vya kufunzishia  tunaiomba serikali  ikumbuke kutenga maeneo ya viwanja vya ndani  vya Judo  (Indoor) kwa sababu huu mchezo unachezewa ndani kama jinsi mnavyoona na pia yanahitajika magodoro  maalumu ya kuchezea ambayo yanahamishika.

"Tuna vifaa vya Judo vimekwama bandarini tangu Aprili 2023 ambavyo  tumepewa msaada na  Chama Cha Judo Dunia ambapo tunadaiwa zaidi ya Mil.Miamoja na nane  ila kutokana na jinsi ushuru kuwa unapanda kila siku itakua imezidi, awali serikali  ilituahidi kutusaidia kutulipia ushuru huo lakoni sasa muda unazidi kwenda hatujaambiwa lolote awali wametupa nguo za mchezo huo zilizokuwa jozi 350 zilizokuja pamoja na  magodoro  ambayo  bado yamekwama bandarini tunaiomba serika ikumbuke ahadi yake ya kutusaidia kupata hivyo vifaa kwani  vitasaidia kuukuza mchezo wa Judo  vifaa hivyo vitagawanywa katika Mikoa mbalimbali nchini" amesema  Katibu Mkuu wa Judo Mallya. 

Amesema kuwa  mchezo wa Judo ni ajira kama zilivyo ajira nyingine  pia  Judo  imeweza kutoa ajira kwa vijana wengi ambao wameajiriwa kwenye Majeshi nchini pamoja na taasisi  mbalimbali, pili Judo ni ulinzi binafsi na ni mzuri kwa afya.

"Hii ni programu ya kuuendeleza mchezo wa Judo kwa watoto malengo ambayo tumeanzisha tangu 2023 na katika  takwimu  zetu zinaonesha  tunawachezaji 508 hadi sasa.
Akitoa salamu za Olympic Tanzania  kwenye ufunguzi wa mafunzo haya  aliyekua mgeni rasmi  Mwenyekiti  wa TOC Gulam Rashid amewataka Makocha hao kuzingatia maelekezo  yote kutoka kwa Mkufunzi huyo Mturuki Erdal Dogan.
Kutoka Kushoto ni  Rais wa Judo  Tanzania  Zaidi  Hamisi Omari , Mkufunzi kutoka UWW  Erdal Dogan  na Katibu Mkuu wa Chama Cha Judo Tanzania  Innocent John Mallya

Post a Comment

0 Comments