Imeandaliwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Habari Tabora United Christina Mwagala
"Hatukutoa mapumziko kwa wachezaji wetu kwa sababu ya kujipa muda mwingine zaidi wa maandalizi, matokeo ambayo tumepata kwenye michezo miwili tuliyocheza ugenini hatukutaka kulala kwakuwa bado tunasafari ndefu ya kutafuta matokeo" amesema Afisa Habari wa timu ya Tabora United Christina Mwagala.
Amesema kuwa ratiba ya timu hiyo ya Tabora United inaonesha kuwa wanamichezo mitatu nyumbani kwa mwezi huu wa Septemba na kwa kawaida tunaweza kusema kwamba ni michezo myepesi kwetu , lakini kwa jicho la kimpira zitakua mechi ngumu sana kwakuwa timu zitakazokuja kucheza wanatufahamu vema uchezaji wa timu yetu , Tabora United tunakikosi kizuri hivyo tunahitaji kuhakikisha tunafanya vizuri ili kuwapa furaha mashabiki zetu.
Tabora United hadi sasa imecheza michezo miwili ugenini na kuvuna alama tatu muhimu huku ikiwa imepoteza mchezo wake dhidi ya Simba na kupata ushindi mbele ya Namungo kwa kupata 2-1 hivyo kuwa kwenye nafasi ya sita ya msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania.
0 Comments