RC PWANI AZINDUA ARDHI KLINIKI MKURANGA

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge  amezindua Kliniki ya Ardhi na Kutatua Migogoro Vikindu katika Kata ya Vikindu,  Wilayani Mkuranga kwa lengo la kusaidia wananchi wa wilaya hiyo kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi inayowakabili.

Uzinduzi wa Kliniki hiyo umefanyika Sept 6, 2024 Kata ya Vikindu ambapo amepata wasaa  wa kusikiliza malalamiko ya wananchi na kutoa mwongozo wa utatuzi kwa kuwataka Viongozi wa Wilaya kufuatilia kwa umakini migogoro hiyo, ili kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa mujibu wa sheria.

Kunenge pia amewahimiza wananchi wa Kata ya Vikindu kujitokeza kwa wingi kutumia huduma za kliniki hiyo ili kurasimisha maeneo yao kwa kufuata taratibu za kisheria.

 "Jitokezeni kwa wingi ili mpate haki ya kukaa kwenye maeneo rasmi," amesema Kunenge.

Aidha  RC Kunenge amewahimiza wananchi kutumia fursa hiyo kutatua migogoro ya ardhi, kwani wapo wataalamu wa masuala ya ardhi ambao wako tayari kuwasaidia.

Baye Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Bi Khadija Nasir amesema kuwa baada ya uzinduzi huo, kambi ya wataalamu itakaa katika Kata ya Vikindu kwa siku nane, ili kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za ardhi zinazowakabili wananchi wa eneo hilo. 

Bi Khadija  amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Pwani  Kunenge, kuongeza idadi ya wataalamu wa ardhi, kwani waliopo kwa sasa hawakidhi mahitaji ya wananchi.
Wataalamu  wa ardhi wakiwa  kwenye Kliniki  hiyo ya Ardhi Vikindu Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Septemba6,2024.
Mkuu wa Pwani Abubakari Kunenge  akizungumza na wananchi  katika zoezi la Ardhi Kliniki  Vikindu Wilayani Mkuranga  Septemba 6,2024.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga  Khadija Nasir akisisitiza jambo kwenye uzinduzi  wa Ardhi Kliniki uliofanyika Septemba 6,2024
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akizindua Ardhi Kliniki Kata ya Vikindu Wilayani Mkuranga Septemba 6,2024.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge  akisisitiza jambo kwenye uzinduzi wa Ardhi Kliniki uliofanyika Septemba 6,2024  Vikindu Wilayani Mkuranga. 
Maafisa Ardhi wakiwa kwenye Kliniki hiyo.

Post a Comment

0 Comments