KANALI KOLOMBO ATOA HAMASA KWA WAZAZI MAFUNZO KWA MUJIBU WA SHERIA

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo akitoa zawadi kwa mhitimu wa mafunzo hayo kwenye sherehe ilifanyika Kikosi Cha 830KJ Kibiti Wilayani Rufiji Mkoani Pwani.

Mgeni rasmi kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu na Maafisa wa JWTZ katika  sherehe za kufunga  mafunzo hayo kwa mujibu wa sheria OP miaka 60 ya Muungano  kikosi 830KJ Kibiti Wilayani Rufiji Mkoani Pwani  yamefanyika 06 Septemba 2024.

"Wazazi  ambao mmefika hapa leo kuwaona watoto wenu wakihitimu mafunzo ya kwamujibu wa sheria Oparesheni miaka 60 ya Muungano muende mkawe mabalozi wetu kwa wazazi wengine wawaruhusu watoto wao kujiunga namafunzo haya" .

Ifahamike kwamba kijana anapojiunga na mafunzo ya kwa  mujibu wa sheria  ni kwamba huku hakuna uonevu wa aina yeyote mtawashuhudia vijana wenu pindi mtakapokuwa nao majumbani mwenu wakirudi kwani wamebadilika tabia na mienendo mbalimbali  waliyokuja nayo, hapa wamefundishwa  kuwa watii, wavumilivu katika changamoto  mbalimbali  watakazokutana  , ujasiriamali na ubunifu.

" Kuna habari za hivyo zinaendele huko mitandaoni kwamba  vijana wakijiunga JKT kuna maovu yanatendeka siyo kweli huu ni uvumi ambao unasambazwa na watu wachache ambao hawana uzalendo na nchi yetu" amesema Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Kolombo 06.Septemba, 2024 katika sherehe ya   kufunga mafunzo  kambi ya 830KJ Kibiti Wilayani Rufiji Mkoani Pwani.

DC  Kanali Kolombo amewaasa wahitimu hao   wa  mafunzo ya kwa mujibu wa sheria Oparesheni  miaka 60 ya Muungano ya kikosi  830 KJ Kibiti  kuzingatia   kiapo walichoapa  kuwa watakuwa watiifu, shupavu pamoja na kuyafanyia kazi  mambo  yote waliyofundishwa wakati wa mafunzo yao ya miezi mitatu.

 "Pamoja na kwamba leo mmehitimu mafunzo yenu ya miezi mitatu kwa mujibu  wa sheria mnapaswa muende mkatii kiapo chenu  kwani mnavyoondoka hapa tambueni kwamba tayari mko katika mfumo  wa orodha ya vijana  waliopita JKT  maana yake ninyi ni wazalendo hivyo kila mmoja aondoke hapa  huku akikumbuka alivyo  apa leo" amesema Mhe. DC  Kanali Kalombo.

Kanali Kolombo ameroa shukran  za dhati kwa Mkuu wa Kikosi cha 830 KJ Kanali Mohammed Bashiri Karuma amesema ameshuhudia namna vijana walivyo onesha  kuiva kimafunzo hata wale ambao wamejaribu kutoroka nao pia wameiva.

Wakati huohuo  ametoa  shukrani  zake za dhati kwa Mkuu wa Majeshi CDF Jacob  John Mkunda  kwa kutoa maelekezo ya kuboresha mafunzo hayo ambayo yametekelezeka.
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Brigedia Jenerali  Solitina  Bernard Mshushi   amewapongeza vijana wote kwa kukubali kuja kujifunza mafunzo haya ya kwa mujibu wa sheria kwa sababu kwa kufanya hivyo wamejitende haki  wenye na katika jamii waliyotoka  na taifa kwa ujumla. 

Mwakilishi wa Mkuu wa JKT Kanali George Barongo Kazahura amewasisitiza  wahitimu hao kuzingatia kuzitunza afya zao ikiwa  ni pamoja na kujiepusha na makundi yasiyo faa kwa sababu JKT  haitafurahishwa kusikia kijana aliyepata mafunzo  yake kwa mujibu wa sheria akikutwa kwenye vilabu vya gongo kujiunga na makundi yasiyofaa na yanayofanya vitendo vya utovu wa nidhamu. 

Post a Comment

0 Comments