NYUNDO NA WENZAKE JELA MAISHA KWA KUBAKA NA KUMLAWITI BINTI WA YOMBO

Watuhumiwa Nyundo na wenzake  waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kumbaka na kumuingilia kinyume na maumbile binti wa Yombo Dovya,  Jijini Dar es Salaam wamehukumiwa kifungo cha maisha jela pamoja na kumlipa faini ya Mil1.kila mmoja  binti huyo.

Hukumu  hiyo imetolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma jana baada ya kuwatia hatiani kwenye mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Washtakiwa  ambao kwenye video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii wakati wakifanya unyama huo wakidai wametumwa na afande walikuwa wanakabiliwa na  kesi ya jinai namba 23476 ya mwaka 2024.

Waliohukumiwa adhabu hiyo ni MT 140105 Clinton Damas, maarufu Nyundo ambaye ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.

Post a Comment

0 Comments