Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani ameahidi kutoa mitungi ya gesi kwa mshindi wa kwanza katika kila timu kwa ngazi ya Kata kwa mashindano ya mpira miguu ya (CCM Cup) yanayondelea.
Na Mwandishi wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani amesema Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imepanga kujenga Kituo cha Afya katika Kata ya Ilolo Mpya, wilaya ya Iringa katika Mwaka huu wa fedha.
“Nawapongeza wananchi kwa miradi ya maendeleo lakini kuna mambo makubwa zaidi yanakuja ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Itunundu kwenda Iringa Mjini ambayo tayari Serikali imeshatangaza tenda, ikiwa ni sambamba na tenda ya ujenzi wa mfereji wa Magoze,” Alisema
Kwa upande wake Afisa Uwezeshaji na Ufuatiliaji wa TASAF Ndg. Salim Mshana amesema majengo yanayotarajiwa kujengwa ni majengo saba ili kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya.
Ujenzi utahusisha jengo la wagonjwa wa nje, jengo la mama na mtoto, jengo la maabara, jengo la upasuaji, jengo la kufulia nguo, jengo kuhifadhia maiti, na nyumba ya waganga ambayo itakuwa mbili kwa moja na njia za kutembelea za kuunganisha majengo hayo .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani pamoja na watendaji mbalimbali katika picha alipotembelea eneo linalotarajiwa kujengwa kituo cha afya katika Kijiji cha Ilolo Mpya.
0 Comments