TAKUKURU WAOKOA ZAIDI YA BIL.1 HALMASHAURI YA KIBAHA

Waandishi wa Habari wakiwa katika mkutano huo.
Kaimu Kamanda wa TAKUKURU   Mkoa wa Pwani Ally Sadiki akizungumza  katika mkutano  na Waandishi  wa Hawapo pichani.

Na Mwandishi  Wetu, Kibaha

TAASISI  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Pwani  wamesaidia kuokoa kiasi  cha Bil.1 ,688,289,634.
09 katika kipindi cha  Aprili hadi Juni mwaka huu.

Yamesemwa hayo leo Agosti 13 na Kaimu Kamanda  wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Ally  Sadiki  amesema TAKUKURU  ilifanya uzuiaji katika ukusanyaji wa mapato upande  wa ushuru wa huduma  katika Halmashauri  ya Mji Kibaha na kufanikiwa kukusanya kiasi hicho cha fedha ambazo awali zilikua zinapotea kwa baadhi  kwa baadhi  ya watumishi kushindwa kufuata sheria,kanuni  na utaratibu za ukusanywaji wa mapato upande wa ushuru wa huduma.

"Katika ufuatiliaji  huo TAKUKURU imebaini kuwa baadhi ya watumishi wa Halmashauri  Kitengo cha ukusanyaji  wa mapato kuwa kuwa  na via sheria vya uvunjifu wa maadili kwa kushindwa kuwajibika
katika ufuatiliaji  nanukusanyaji wa ushuru wa huduma.

Amesema  kuwa baadhi ya  watumishi kuingia  makubaliano na wafanyakazi  katika kulipa ushuru wa  huduma na kuwaruhusu kulipa kiasi kidogo ukilinganisha na mauzo yao halisi.

Baadhi  ya Wafanyabiashara  wanapotaka kulipa  ushuru wa  huduma wanajikadiria mauzo yao hivyo  kusababisha kulipa ushuru wa huduma kiasi kidogo  ukilinganisha  na  mauzo halisi kutoka kwenye Z-REPORT kama sheria  inavyowataka kutumia Z-REPORT katika kukokotoa mauzo"amesema Kaimu Kamanda TAKUKURU Sadiki. 

Amefafanua  kwa kusema kuwq  baadhi ya Wafanyabiashara  kulipa  nusu au hawalipi kabisa ushuru wa huduma kwa madai kwamba  Kibaha ni eneo la uzalishaji
(Viwanda) na siyo  eneo  la mauzo (Sokoni), hii ni kutokana  na wafanyakazi kutokuwa na elimu ya kutosha  kuhusiana  na malipo ya ushuru wa huduma huku baadhi ya Wafanyabiashara  wamegundulika kuwa wanamiliki mashine za EFD zaidi ya moja hivyo  kuficha  zingine  ili kukwepa kulipa kiasi sahihi anachotakiwa kukilipa.

Kaimu Kamanda  TAKUKURU Mkoa wa Pwani  Sadiki  ameongeza  kwa kusema kuwa taasisi hiyo imesaidia kuongeza makusanyo  hayo baada  ya kushirikiana  na Mkurugenzi  wa Halmashauri  ya Mji Kibaha baada ya  kuonekana  mapato yaliyokusanywa awali kwa robo ratu za mwanzo kwa mwaka wa fedha   kati ya 2023  na 2024 ni ndogo  kulingana  na vyanzo vya mapato  vilivyopo ndani ya Halmashauri. 
"Katika kipindi tajwa tumefanya uchambuzi wa mfumo mmoja  katika  eneo la ukataji wa kodi ya zuio katika miradi ya maendeleo  Halmashauri  ya Kibiti" amesema  Kaimu Kamanda TAKUKURU Mkoa wa Pwani Sadiki.

Aidha kwa upande wa ufuatilia wa utekelezaji  wa miradi ya maendeleo  tayari wamefuatilia.kiradi kumi yenye thamani ya Bil.10,619,073,893.77 katika sekta za Elimu, Maji,TANESCO, Afya,Ujenzi ,barabara  na biashara  kati ya miradi hiyo hakukuwa na mradi ulioonekana kuwa na mapungufu.
Wakati huohuo  TAKUKURU Mkoa wa Pwani imeendelea na utekelezaji wa program  ya TAKUKURU Rafiki na kuzifikia  kata sita  huku kero zilizoibuliwa  na kupatiwa ufumbuzi zimetoka Idara ya Jeshi la Polisi, Utawala  ,Afya , Elimu,Ardhi,TANESCO na Barabara.

Kaimu Kamanda Sadiki amesema kuwa  katika kipindi taja juu wamepokea  malalamiko  95 huku kati ya hayo malalamiko 55 yamehusu rushwa na taaifa hizo zimeshughulikiwa kwa mujibh wa sheria  kwa kuanzia uchunguzi ambao upo katika  hatua  mbalimbali  za uchunguzi. 

"Taarifa 40 zilizobaki ambazo hazikuhusu rushwa zimeshughulikiwa kwa njia  ya uelimishaji,uzuiaji ushauri nankuhamishiwa idara nyingine,  taarifa hizo zimepokelewa kwa Mchanganuo  ufuatao  TAMISEMI 22,Mifugo/Uvuvi3,Elimu 14,Polisi7,Ardhi12,Fedha3,Maji2,Mahakama 5,binafsi9,
Ujenzi6,Afya7,
Siasa moja,Manunuzi moja,Maendeleo ya jamii moja,Kodi/  Mapato  moja.

Katika kipindi hiki TAKUKURU Mkoa wa Pwani  imefungua  jumla  ya kesi mpya 11 Mahakamani  huku kesi saba  wametiwa hatiani.

Akizungumzia kuhusu  namna walivyojipanga  na vitendo vya rushwa  katika uchaguzi, "Mkoa wetu una ofisi  tisa katika Wilaya  zote  kuna jumla ya Kata 133,Mitaa 490 na Vitongoji 2029, kwa kipindi hiki tumeshaanza kufanya  ufuatiliaji  wa vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika baadaye mwaka huu". 
Mwisho Kaimu Kamanda Sadiki ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani kuendelea  kuunga  mkono  jitihada za kufichua vitendo vya rushwa  na wala rushwa kwa kutoa taarifa sahihi  zitakazowezesha kuwachukulia hatua  wahusika hasa katika kipindj hiki tunapoelekea uchaguzi wa serikali za  mitaa na amewasisitizawananchi waonunua  maeneo  wahusishe  serikali za mitaa  na kufuata sheria na kanuni na taratibu ili kuepusha migogo ya ardhi inayojitokeza mara kwa mara na kwenda na kauli mbiu isemayo kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu tutimize wajibu wetu.
Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo.

Post a Comment

0 Comments